Historia-Queens Fc ndiyo Simba ya leo

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,391
36,518
SIMBA SC NI ZAO LA YANGA SC

Jambo moja ambalo wengi hawalijui ni jinsi Yanga na Simba zilivyotokea na chanzo cha upinzani wao mkali.

Mwaka 1928 Yanga ya sasa ilijulikana kama ' the Navigators ' wakitumia jezi za blue bahari ; ikiwa moja ya timu pekee yenye nguvu ya wazawa mbele ya timu nyingi za wakoloni.

1930 Yanga ikizidi kupata picha na taswira ya uzalendo ilibadilishwa jina na kuitwa ' New Young ' ikizisumbua sana timu za Serikali na wakoloni wake na kuzidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa watanganyika na wapigania Uhuru chini ya TAA.

Tarehe 11 February, 1935 Yanga ilibatizwa rasmi jina la Dar es Salaam Young Africans lakini miezi 12 baadae ndani ya timu ulizuka mgogoro mkubwa na baadhi ya viongozi kujitenga na kuanzisha timu nyingine kupingana na Young Africans iliyoitwa Queens FC ambayo ndio Simba SC ya sasa baada ya kupata jina hilo mwaka 1971 .

Leo Yanga inatimiza miaka 84 na baadae August 8, Simba SC watatimiza miaka 83.

Mafanikio ya Yanga SC

Imetwaa kombe la ligi kuu mara 27 wakiwa mabingwa wa muda wote , CECAFA mara 5 na FA ( ASFC ) mara 4 .

Mwaka 1969 miaka minne tu baada ya kuanzishwa ligi daraja la kwanza nchini ; Yanga walifanikiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika na kuishia hatua ya robo fainali pia mwaka uliofuata mwaka 1970 katika michuano hiyo waliishia tena hatua ya robo fainali.

Kombe la Washindi barani Afrika mwaka 1995 waliishia hatua ya robo fainali.

Yanga SC walianza kutumia rangi zao za manjano na kijani mwaka 1948 wakiachana na rangi za blue bahari zilizokuwa zikichanganywa na weusi . Rangi ya blue bahari bado wanaienzi kwa kutumiwa na makipa wao au bips za mazoezini.

Pichani ni kikosi cha Yanga SC mwaka 1974 kilipofanya ziara nchini Brazil na hapo wapo katika uwanja maarufu wa Maracana.
FB_IMG_1549887601007.jpg

Copy and paste
 
Back
Top Bottom