Historia Fupi ya wazee wa Abdul Nondo

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
516
2,876
By Hamis Hababi.


Kijana huyu Abdul Mahmoud Omar Athuman Kagobe, (Abdu Nondo) ni mjukuu wa Omar Athuman Kagobe, ambaye ni veteran wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1914 – 1918), na baadae alijiunga na Jeshi la Polisi na kuacha kazi baada ya uhuru, mwaka 1961.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndiye aliyeileta TANU Ujiji na nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndio pia alipofikia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bibi Titi na Sheikh Suleiman Taqadir mara mbili kwenye harakati za kupigania uhuru na mahali hapo ndio TANU imejenga Mnara wa Kumbukumbu.

Kwenye nyumba hiyo ndio pia alipofikia Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy mara mbili na Sheikh Hassan bin Ameir.

Dada yake Mzee Omar Athuman Kagobe ni Zubeda Athuman Kagobe aliyeolewa na Muhindi Taki aliyekuwa na uwezo uwezo kipindi hiko ,wakati Nyerere alipokwenda kigoma alitafutiwa sehemu nyumba ya watu wenye uwezo kidogo anapelekwa kwa Zubeda Athumani Kagobe ,Dada wa babu wa Abdul Nondo, aliyeolewa na Muhindi Taki Nyerere alipokuwa anakula akaulizwa "Vipi nafasi ya Machotara na wenye mali tunasikia wayanyanganywa mali zao ,Nyerere akajibu *hapana tutatengeneza Tanganyika yenye usawa*

zubeda ndio aliyemzaa Dr. Sherry Taki, msomi wa sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Lumumba, Moscow wakati wa Urusi ya Kikomunisti ndiye baadaye Nyerere aliwakumbuka famalia ya Taki baada ya uhuru na kumchukua Mtoto wa Zubeda na Taki anaitwa Dr.Sherry Taki katika Baraza la ushauri wa Rais Nyerere baadaye akawa mjumbe wa NEC ya TANU.

Mwanae mwingine ni Mamdu Taki, msomi wa Tabora School na Makerere alikoma pamoja na akina Timothy Apiyo, na akafanya kazi Mamlaka ya Tumbaku kwa zaidi ya mianka 20.

Binti yake Nargis Taki aliolewa na Mpigania uhuru wa Tanganyika Bwana Rashid Kheir Baghdellah, ambaye ametajwa sana kwenye Kitabu cha Mohmed Said, mwandishi wa kitabu cha ‘’Maisha na Nyakati ya Abdul Wahid Sykes…’’ Bibi yake mzaa baba ni Kulthoum Hemed Kiumbe, dada wa Sheikh Khalfan Mohamed Kiumbe, na Mahmoud Mohamed Kiumbe ambaye alikuwa mwanachama shupavu wa TANU na kabla ya uhuru Mtaa Maalum ulipewa jina lake huko Ujiji mpaka leo, unaitwa Mwalim Kiumbe Street.

Babu yake Mzaa mama ni Alhaj Juma Rehani, msomi kwenye Tarika ya Mwinyi Mkumbati, Twarika ya zamani sana Ujiji iliyoasisiwa na Mwinyi Kheir Bin Mwinyi Mkuu Al Ghashan, mkubwa wa zamani wa Ujiji akiwakilisha Dola ya Zanzibar, ikisimamiwa na Sheikh Hamisi Bin Sali, na ikarithiwa na Salim Bin Mwinyi Kheir, ndiyo ikaja kusimamiwa na Mwinyi Mkumbati.

Akina Sheikh Kiumbe walikunywa ijjaza kwa Sheikh Khalfan Al Bulush mrithi wa tarika hiyo ambayo ilikuja kurithiwa na Sheikh Kiumbe na Sheikh Omar Kakolwa na kupata nguvu alipokuja Sheikh Mohamed Nassor kutoka Zanzibar, babu yake Abdu Nondo na aliendelea kuwa Khalifa wa Sheikh Mohamed Nassor kwenye Tarika Qadiria hadi umauti.

Mama wa bibi Abdul Nondo (kuruthumu Hemed kiumbe) Mama yake anaitwa zuhuru ambaye baba wa zuhura anaitwa mzee burega (BUREGA),mwenye jina la BUREGA -Ujiji ,Mzee Burega alimzaa pia Mzee Fikirini ambaye ni marehemu ! Maeneo yote ya burega yalikuwa mashamba ya Mzee Burega kipindi hiko ndio watu walianza kuhamia akawa anawakatia ardhi.


Kadhia ya Abdul Nondo inatukumbusha zamani tu baada ya Tanganyika kupata uhuru, mwaka 1968 Mwalim Kambarage Nyerere alimtuma Aliyekuwa Waziri Wa Mambo ya Ndani Saidi Maswanya, kuwataka watu wa Kigoma wathibitishe Uraia wao, wakiwemo wanafunzi waliotoka Mkoa Wa Kigoma popote walipo walirejeshwa makwao kwa ajili ya zoezi hilo,

Kwenye mkutano Bwana Said Maswanya, aliambiwa na wazee wa Ujiji wakiongozwa na Alhaj Yussuf Tossir na Mzee Rashid Kazema, akamwite aliyemtuma na mkutano ukavunjika, na hii ndio lilipelekea Mhesimiwa Manju Msambya na marehemu Aman Walid Kabourou kufanyiwa fitna na kufukuzwa shule Kigoma Secondary Nyakati hizo.

Ombwe hili ambalo la kibaguzi lingalipo linawaandama wenyeji wa Kigoma mpaka sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam, natumai wale waliokueleza ukalete vyeti vya babu zako wakisoma huu waraka sijui wanajionaje. Pole sana na kadhia ilokupata. Mungu akutie nguvu na uangavu wa kifikra ili ufikie ndoto zako
 
Mzee Rashid Kazema,


Kwakweli ni historia nzuri sana na yenye ukweli kabisa, na watu itabidi wajifunze.

Ila ningependa kuleta masahihisho kidogo katika jina; sio Mzee Rashid kazema ni Mzee Bakari Kazema ambaye ndiye Baba wa Rashid Kazema.

Akhsante.
 
Back
Top Bottom