NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,032
- 4,028
Kuanzia leo nakuendelea nitakuwa nawaletea majina ya mataifa ya Afrika alphabetically na historia ya waasisi wa mataifa hayo.
1.ALGERIA.
Ahmed Ben Bella alizaliwa 25 Dec 1916 alimuoa Zohra Sellani
alikuwa mwana siasa,mjamaa, askari,mwanamapinduzi alikuwa ndio raisi wa kwanza wa Algeria mwaka 1963-1965.
Alizaliwa sehemu inaitwa Maghnia kipindi cha utawala wa kifaransa,mtoto wa mkulima.Alihuhudhuria shule Ufaransa huko ndiko akaja gundua ubaguzi mkubwa kwa waarabu toka kwa walimu wake wa kifaransa.Alianza kulalamika na kukandia hali hiyo ya ubeberu na ukoloni na alipinga utamaduni wa kigeni kwa taifa lake na mara moja akaanza kushiriki harakati za utaifa.
Alijitolea kwenye jeshi la Ufaransa mwaka 1936.Alipigana vita vya pili vya dunia upande wa mfaransa.
Hata hivyo watawala walimuona ni mwiba mchungu wakatuma muuaji kwenda kumuua kwenye shamba lake.Jaribio hilo liliposhindikana wakaamua kutaifisha shamba lake.
Aliunda chama cha (OS) Organizationale Speciale kwa madhumuni ya kuchukua silaha dhidi utawala dhalimu wa kifaransa.
Hii ilileta kuundwa kwa NLF National Liberation Front mwaka 1949.
Alivunja bank mji wa Oran ili apate fedha za kuendesha chama lakini alikamatwa na kupelekwa gereza la Bilda mwaka 1951 na kuhukumiwa miaka 8.Alifanikiwa kutoroka na kukimbilia Tunisia mwishowe akafika Cairo mwaka 1952.
Vita vya Algeria vilipoanza 1954 alikuwa makazi yake ni Cairo akiwa ni mmoja wa wanachama wa kamati ya umoja kitendo ambacho kilikuja kuzaa (FLN) Front de Liberation Nationale ambapo kilizaliwa November mwaka huo.
Nia ya kumuua bado mabeberu walikuwa nayo mwaka 1956 alipokea kifurushi kutoka kwa driver tax akiwa hotelini Cairo akakataa kukipokea dereva alipoondoka tu na kifurushi hicho bomu likalipuka na kumuua dereva.Baadae akiwa hapo hapo hotelini Cairo alikuja mtu na bunduki akafyetua risasi haikumuua ila ilimjeruhi kidogo lakini mshika bunduki huyo aliuwawa na walinzi akijaribu kutorokea mpaka wa Libya.
Alikuwa anaunga mkono harakati nyingi za kudai uhuru kwa mataifa mengine.Ikumbukwe Mandela alipitia hapa Tanzania akaacha viatu vyake Dar akaelekea Algeria kupata mafunzo ya kijeshi kupambana na Makaburu ndipo aliporudi akafungwa maisha.
Ben Bella pia alikutana na Fidel Castrol na Che Guevara Havana Cuba mwaka 1962.Pia alikuwa anaungwa mkono na Pakistani.
Alichaguliwa kuwa raisi wa kwanza wa Algeria mwaka 1963.
Alipinduliwa na mkuu wake wa jeshi Boumedienne mwaka 1965.
Alifariki 11 April 2012
Somo lijalo tutaangalia nchi ya BENIN
Itaendekea
Sent using Jamii Forums mobile app