Hispania yakataa tangazo la uhuru la Catalonia

Hispania yakataa tangazo la uhuru la Catalonia

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322

_98260711_gettyimages-859859172.jpg

Wale wanaounga mkono uhuru walikusanyika Barcelona

Serikali ya Hispania imekataa tangazo la kujitangazia uhuru lililotiwa sahihi na kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na kutupilia mbali wito wa kutaka kuwepo mazungumzo.

Naibu waziri mkuu wa Hispania amemtaja Bw Puigdemont kama "mtu asiyejua yuko wapi au kile anachokifanya".

Waziri mkuu Mariano Rajoy, anafanya mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kuzungumzia hatua ambazo serikali itachukua.

Mr Puigdemont alitia sahihi tangazo la uhuru siku ya Jumanne, lakini akazuia kutekelezwa kwake ili kutoa nafasi kwa mazungunzo.

Kumekuwa na uvumi kuwa rais huyo wa Catalonia anaweza kutangaza uhuru na kutekeleza hatu hiyo yake ambayo itaiweka Hispania katika hali ngumu kisiasa.

Akihutubia bunge la Catalonia mjini Barcelona siku ya Jumanne, Bw Puigdemont alisema kuwa ene hilo linalojitawal,a lilipata haki ya kuwa huru kutokana na kura hiyo.

"Tunatoa wito kwa mataifa ya nje na mashirika kutambua taifa la Catalonia kama tafa huru," alisema.

Yeye na viongozi wengine wa Catalonia kisha wakatia sahihi tangazo la uhuru. Haifahamiki ikiwa tangazo hilo limeambatana na sheria.

Umati unaouga mkono Uhuru mjini Barcelona ulisherehekea matashi yake Bw. Puigdemont, lakini wengi wakaelezea kughadhabishwa wakati alielezea kwa kina msimamo wake.

Chanzo: BBC
 
duu hi nayo kalii kwani wakiwapa uhuru wanapungukiwa nini watu hawataki muungano wana wakatalia wanini ,mi nawaomba wakatalunya wakomae hivo hivo mpaka uhispaania waeleweke vivaa vivaa katalunya.
 
duu hi nayo kalii kwani wakiwapa uhuru wanapungukiwa nini watu hawataki muungano wana wakatalia wanini ,mi nawaomba wakatalunya wakomae hivo hivo mpaka uhispaania waeleweke vivaa vivaa katalunya.
Haki zina mipaka,uwezi kuamka Leo,ukasema Arusha,ijitenge na TZ,itabidi tukutandike tu,
Uwezi kukurupuka asubuhi,ukasema Gesi yetu haitoki,ibaki hapahapa Ntwara!!,tunakutumia Vijana,wa makutopora,wakutwange,wakishirikiana na wenzao,wa pale nachingwea,ili ushike adabu,
Walevi wengine,oh eti tuiache zenj,iende,iende wapi,hiyo sio haki ya wale tu wanaotaka kujitenga,hata wale wanaotaka kukimbiwa,wanahaki,ya kuhoji,
Hispania,twanga hao katalonia,mpaka washike adabu,hiyo ni nchi mmoja,
Nenda America,useme Texas,ijitenge na USA,uone,utakachofanywa,
Life is not black and white,there are glay areas,
 
Urusi nchi ngapi zilijitenga?
 
Ishu ya urusi ni pana sana,ilikuwa ni kipindi cha vita baridi,ukomunisti,na ubepari,hizo nchi ziliamua kujiondoa sio kwa sababu,ziliona hakuna maendeleo katika umoja,USA,kupitia mashirika yake ya ujasusi,yalichangia,KGB,ilikuwa na sera duni,ambazo ilifika pointi,was soviet wakaacha kuziamini,walipokuwa wakijiringanisha na nchi za kibepari za magharibi,na hizi nchi zilikuwa kwenye umoja kwa kuunganishwa na itikadi ya kikomunisti tu,itikadi iliposhindwa kutatua changamoto za maisha,nchi wanachama,wakaanza kujitenga,wakisaidiwa na America,unaukumbuka ukuta wa Berlin,ulipoangushwa,wa German,wakaona ni bora kuungana,hakuna maana ya kuwa na west na East German,
UK,ambo ni muungano wa nchi kadhaa,kuna nchi mojawapo walitaka kujitenga,ikapigwa kura ya maoni,unajua kilichotokea,UK bado ni moja.
 
Back
Top Bottom