Njia mojawapo ya kupunguza au kuondoa tabia fulani ni kuondoa mazoea.
Mwanaume anaweza kuanza kuchepuka, kadiri atakavyoendelea, atajenga tabia, akijenga hiyo tabia baadaye ataona jambo hilo ni la kawaida. Akishafikia hatua ya kuona jambo hilo ni la kawaida, wala hataumizwa katika moyo wake hata pale anapofanya.
Mazingira wakati fulani huchangia urahisi wa kupotoka. Kama unadhani mumeo ni dhaifu, jitahidi sana kila muda kuwa na mumeo mpaka ifikie mahali kila mmoja aone kuwa mnahitajika kuwa wote karibia kila mahali wakati wote. Mazingira hayo yatakuwa siyo mazingira rafiki. Na hata wale wenye kumpigia mahesabu mumeo wataona kuwa mumeo siyo mtu wa kupatikana kiurahisi.
Baadaye mumeo anaweza kujenga mazoea ya kuwa nawe wakati wote, na pia kujenga mazoea ya kutokuchepuka, na akitokea kuchepuka akitoka huko kwenye mchepuko lazima atakuwa hana amani na dhamira itamshtaki, na mwanaume anayesutwa na dhamira ni rahisi sana kujutia alichokifanya, na kukiacha. Lakini ni kweli pia kwa baadhi ya wanaume hata ushauri huu unaweza usifanye kazi.
Wenzetu wazungu, tabia ya kila mara mume na mke au boyfriend na girlfriend kuwa pamoja imepunguza sana tabia za kuchepuka.