Hisia na hamasa za Maandamano nchini: Mapokeo, Mitazamo na Uhalisia (Viongozi na Wananchi)

Mange Kimambi kwa kumbukumbu za mwisho likuwa mwanachama wa CCM.
Sijui nini kimemsibu hadi kuanzisha wazo la maandamano, lakini kwa mantiki ya karibu anajipotezea wakati.

Mange kwanza hayupo nchini, hivyo basi sababu za kuanzisha maandamano wakati akionyesha uoga wa kutokuwepo nchini haileti maana.
Pili, hata kama kuna kutokuridhika na jambo fulani, kuna njia mbadala kufikisha ujumbe hata kama walengwa hawapendi.
Tatu, baada ya maandamano tutegemee nini?
Watu watarudi majumbani na kutafuta ugali wale, walale.
Nne, matusi, mengine ya nguoni kwa viongozi hayampi heshima Mange wala umaarufu wa kuwa kiongozi mwenye heshima au kiongozi mbadala.
Tano, kwa matusi ya nguoni yanayomporomoka Mange, wanaomuelewa ni vijana wa vijiweni au vijana wahuni.
Sita, Mange anayajua matatizo kwa vile analetewa matatizo hyo. Lakini yeye mwenyewe hajui wala hana idea au vision ya kule watanzania anataka waende wapi. Kuonyesha matatizo sawa, lakini utatuzi wa matatizo hayo ni usiku wa giza kwa Mange.
Saba, siku ya tarehe 26 April tutaamka watanzania na tutalala watanzania kama kawaida.
alipokuwa anaipigia kampeni CCM alikuwa anaishi Dodoma au Gongo la mboto ??
 
wapuuzi hawa ... nikiwatizama sioni mwandamaji hata mmoja.. wanatupigia tu kelele na kutukana kila wakati lakini labda wataandamana majumbani kwao na nyuma ya keyboards.
Kwani unataka waandamane? Mm sioni sababu ya kushupalia pointi ya hakuna wa kuandamana labda iwe nyuma ya keyboard ilihali wewe hutaki maandamano. Au unayataka maandamano sema unaona watu ni waoga hawawezi hivyo unawatia hasira ili waonyeshe wanaweza? Ungejikita kwe kutoa elimu ni kwann wewe hutoandamana ningeona hapo Una Nia ya kuwashawishi watu waachane na mawazo ya maandamano. Ila unavyoongea ni kama unataka wakuprove kuwa wanaweza na hawaogopi.
 
Mwisho wake unakaribia
IMG_20180226_235953.JPG
 
Nikiwa mmoja wa waandamanaji naomba nikujibu kwa niaba ya kundi kuuubwa la vijana wenzangu tunaochoma mahindi hapa stendi ya mabasi yaendayo DSM

1. Mimi na wenzangu tunatakiwa kuandamana kwa sababu tunahitaji mabadiliko ya KATIBA na pia kumtaka Malaika Jiwe atupishe yeye na familia yake katika kiti cha uongozi wa nchi hii

2. Naandama kuanzia na kuishia kwenye eneo litakalo create attention ya sisi kusikilizwa matakwa yetu yaani tunasimamisha nchi

3. Mwisho wa maandamano ni pale matakwa yetu yatakapo timizwa

4. Nimejipanga kuvumilia maumivu ya kipigo na kashkash zitakazo jitokeza mwanzoni ambazo badae zitakwisha kwa sababu woote tutaungana ukiwemo wewe hata hao polisi watatu support then wakati huo na wewe utatusupport ukiwa tayari umesha unganishwa na network ya VVU

5. Anaye tuhamasisha tuandamane yeye ataongoza maandamano hayo akiwa DC Washington Marekani ... upo hapo Nyonyo!!

Najua mtu Kama wewe huwezi kuandamana kwa sababu una uhakika wa kula, unauhakika wa kuangalia TV Kama ulivyosema utakua unabadilisha channel tu, una uhakika wa kimshara mbuzi labda unachopata kwa hako ka kazi ulikounganishiwa na baba ako mdogo ...

Sisi wagubi wachoma mahindi lazima tuandamane kwa sababu hatuna uhakika wa kula katika maisha yetu, hatuna TV wala zile flati skrin tuaziona kwa wenzetu tu, hatuna ajira Wala ndugu wa kutuunganisha kupata ajira ...

Amini usemi usemao Alie Shiba hamjali mwenye njaa ...
Huku kwetu sa hivi maindi ya kuchoma na pilipili yanalipa sababu ya baridi. Unaweza funga hesabu hata 30th per day. Anyway, Maelezo yako yanaonyesha kwamba kinachokufanya uandamane ni njaa na umaskini. Tatizo ni kwamba hata nchi zenye nguvu na demokrasia ya kiwango cha juu bado kuna wenye njaa na maskini. Mange atakuwakilisha huko alipo Ila kule kwao polisi hawajui kugawa dozi, na pale wanapogawa hospitali zao zinajiweza. Nimetaka tu ulifahamu hili halafu nikutakie kila la heri unapojiandaa kupambana na dola. Kumbuka, hamnaga jambo rahisi. Kupambana na dola ni ngumu na hatari kuliko kuchoma mahindi. Best of luck kamanda.
 
kila siku ya mapinduzi miaka ijayo,kumbukumbu zenu zitamkumbuka Mange Kimambi,mnadhani yeye mjinga ??
Watz huikumbuka hii siku sababu hawaendi Kazini. Sidhani ka wanajali kuhusu mapinduzi au nani alimpindua nani. Labda kama maandamano yatokee yasipotokea watachekana hiyo tarehe af huko mbeleni litakuja lingine hili litasahaulika. Maisha ya waTz wanayajua waTz wenyewe.
 
Mange Kimambi kwa kumbukumbu za mwisho likuwa mwanachama wa CCM.
Sijui nini kimemsibu hadi kuanzisha wazo la maandamano, lakini kwa mantiki ya karibu anajipotezea wakati.

Mange kwanza hayupo nchini, hivyo basi sababu za kuanzisha maandamano wakati akionyesha uoga wa kutokuwepo nchini haileti maana.
Pili, hata kama kuna kutokuridhika na jambo fulani, kuna njia mbadala kufikisha ujumbe hata kama walengwa hawapendi.
Tatu, baada ya maandamano tutegemee nini?
Watu watarudi majumbani na kutafuta ugali wale, walale.
Nne, matusi, mengine ya nguoni kwa viongozi hayampi heshima Mange wala umaarufu wa kuwa kiongozi mwenye heshima au kiongozi mbadala.
Tano, kwa matusi ya nguoni yanayomporomoka Mange, wanaomuelewa ni vijana wa vijiweni au vijana wahuni.
Sita, Mange anayajua matatizo kwa vile analetewa matatizo hyo. Lakini yeye mwenyewe hajui wala hana idea au vision ya kule watanzania anataka waende wapi. Kuonyesha matatizo sawa, lakini utatuzi wa matatizo hayo ni usiku wa giza kwa Mange.
Saba, siku ya tarehe 26 April tutaamka watanzania na tutalala watanzania kama kawaida.
(NB
MODS mliisweka na kuunganisha na nyingine mada hii, hivyo kuipotezea.
Tabia hii haina tofauti na serikali inapolipiga marufuku gazeti kwa kutoa maoni yake
.)
 
Hivi serikali haijiskii vby kuwa na hofu hadi polisi kufanya mazoezi makubwa hivyo kwa ajili ya kale ka-dada Mange? Je wangekuwa ni akina lowasa, mbowe au Lissu ndio wametangaza maandamano si ndio hadi JW wangekuwa wanaruka na ndege za kijeshi kujenga hofu?
 
Baadhi ya watu wanamuona mange chizi ila yote anayoyapinga kuhusu hii serikali ni ukweli mtupu na maandamano yatafanikiwa vibaya mnooo tukutane tarehe 26/04 maandamo oyeeeeee
ni chizi kweli na kawashika vichwa machizzi wenzake kama wewe,jaribuni muone cha moto mtajuta kuzaliwa.
 
Baadhi ya watu wanamuona mange chizi ila yote anayoyapinga kuhusu hii serikali ni ukweli mtupu na maandamano yatafanikiwa vibaya mnooo tukutane tarehe 26/04 maandamo oyeeeeee
Mange sio chizi kwani? Basi ni kichaa
 
Back
Top Bottom