HIMARS ni nini?

HIMARS ni nini?

Mavindozii

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
2,110
Reaction score
2,786
Kiufupi
HIMARS ni mfumo mzima wa kurusha maroketi pia Makombora.

Ina Rocket za M31 ambazo ndo Ukraine imepewa, zina range 80km.
Pia inaweza kurusha Makombora makubwa kama Army Tactical Missile (ATACMS) ambalo hili linakwenda umbali Hadi 300km likiwa na mlipuko mkubwa zaidi,hili tunaweza fananisha na kombora la Urusi linaitwa Iskander.
Na sasa wanatengeza kombora jipya "Precision Strike Missile" nalo litarushwa kupitia HIMARS,zitaanza kutumika kuanzia mwakani Range yake ni 500km.

Himars sio mfumo mpya Marekani imeutumia Sana kwenye vita ilizopigana Kama kule Iraq, Afghanistan,nk. Kinachofanya iwe deadly ni uwezo wake wa kurusha Makombora na kukimbia,wenyewe wanaita Shoot and Scoot (Unaweza Rusha Maroketi yote sita ndani ya sekunde 20 na kukimbia). Hivyo ni vigumu Kwa adui kujua mfumo upo wapi pia si rahisi kwa adui kuziharibu,ndio maana ikaitwa High Mobility Artillery Rocket launchers System (HIMARS).

Maroketi yake Yana speed Sana yanakimbia Kwa Kasi ya mara mbili zaidi ya sauti (Mach 2) hayafuati ballistic trajectory pia yana Radar cross section ndogo hivyo inakua ngumu kwa mifumo ya adui kuyatungua ndio maana unaona kule Ukraine maghala ya silaha ya Urusi na command posts zinalipuliwa na HIMARS na air defense system zinapata taabu kuyadaka haya maroketi.

Maroketi yake yanatumia GPS kufikia target. Na Kama ikatokea GPS imekua jammed pia yana uwezo wa kupiga target kupitia INS.
 
Ni mwendo wa kipigo tu hakuna namna
JamiiForums-243801660.jpg
 
Back
Top Bottom