Hillary Clinton kutogombea tena

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,520
9,322
Hillary Clinton ametangaza kuwa hatowania urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Akizungumza katika kituo kimoja cha televisheni mjini New York ,Hillary Clinton amesema kuwa ataendelea kuunga mkono na kufanyia kazi kile anachoamini kuwa ni sawa bila ya kushiriki kama mgombea katika uchaguzi ujao.

Kiongozi huyo ameongeza kwa kusema kuwa anasikitishwa kwa kile kinachoendeela nchini Marekani na kwamba jambo hilo linamtia wasiwasi mkubwa.

Hillary Clinton ni mwanamke wa kwanza kuwania urais kupitia chama cha Democratic katika historia ya Marekani.

Mpaka sasa wagombea waliojitangaza kutoka chama cha Democratic ni Bernie Sanders,Elizabeth Warren,Cory Booker na Kamala Harris

Muungwana
 
Dhulma ndiyo iliyomponza, ile ilikuwa nafasi ya Bernie, mzee wa watu akadhulumiwa hivi hivi na Mungu si athumani, akajidhihirisha, hata kama ni kwa Trump.
 
Back
Top Bottom