Hillary Clinton aiumbua Tanzania

Pamoja na kupigia debe ziara yake alipokuwa hapa mama huyu, na kuwa ameamua kufuta umasikini, Bi Clinton aweka wazi kutokuridhika na hatua za kimaendeleo zilizofikiwa na Tanzania.

Akitoa majumuisho juu ya ziara yake katika nchi kadhaa za Africa, Hillary alitumia muda mwingi kuisifia na kuipongeza Rwanda, kwa hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa, hatua ambazo zimeipeleka nchi hiyo kuelekea kujiondoa katika nchi masikini. Alizitaja nchi nyingine zilizopiga hatua kimaendeleo kuwa ni Zambia, Mali na Ghana. Hakuitaja kabisa Tanzania katika nchi zilizoonyesha juhudi za kupiga hatua kimaendeleo

Source; ITV

Soma kwenye nyekundu, kwa hiyo hayo mengine yote kuhusu kuiumbua Tanzania ni porojo zako?
 
Kwa hiyo Chadema-JF, mmejifariji kwa kutoitaja Tanzania?

Inaonekana ndg swala la nchi na u-Tanzania kwako ni tatizo kubwa sana.Hivi lini mtaacha kuugua huo ugojwa wa kuhisi CHADEMA wanataka hivi,wanataka vile...? We need Tanzanins here;watu wenye uchungu na hii nchi na siyo ushabiki wa kipuuzi always. CCM Helps nothing here na wala watu hawaichukii kwa sababu ni CCM. Hawaitaki coz ni ya kihuni,ina sera za kienyeji ambazo tangu UHURU mpaka leo zimetufikish hapa! Tunafikiri hawa ni vipofu na wanatakiwa kupumzika for now ili wawapishe wengine wawaelekeze namna ya kongoza nchi na kugawa resource kwa priorities
 
chatu dume;Mbona tunakuwa watumwa wa kiakili, Marekani wapo kimaslahi popote unapowaona nchi wanazosifia ni kwa faida yao sio faida ya Africa

Mkuu utumwa wa akili uko wapi mtu kukutolea mifano ya jirani zako walivyopiga hatua? Masilahi ya US kwa kuzitaja hizo nchi jirani zetu inahusiana vipi na sisi kuonekana hatujapiga hatua? Ukweli unauma au ni chuki yako juu ya US? Kwa mtizamo wako unaona tumepiga hatuwa katika nyanja zipi ambazo unaweza kumuonyesha mtu yeyote? Mkuu huoni nchi hii ipo katika hali mbaya sana kiuchumi na watanzania wengi wana maisha magumu? Acha ushabiki, hapo ulipo tafakari Tanzania imepiga hatuwa zipi kwa miaka mitano iliyopita kimaendeleo. Majibu unayo nadhani mkuu.
 
Kweli baada ya Damu kumwagika Rwanda; Sasa ni Nchi Bora hata zaidi ya Tanzania?

Kumwaga damu ni bora zaidi ya UFISADI WA CCM
 
Back
Top Bottom