Cardinal06
JF-Expert Member
- Jan 7, 2015
- 963
- 327
Kuna tangazo huwa linarushwa ITV kabla ya taarifa ya saa mbili usiku, tangazo hili linahusu Uzazi mpango, tatizo langu sio katika ujumbe wa tangazo hili bali ni wahusika waliotumika. Wametumika watoto wadogo ambao wana'act kama wapiga kampeni na wanataka kuwaambia wazazi watumie Uzazi wa mpango.
Wadau hii ni sawa? Mtoto- hasa wa umri kama uliotumika katika tangazo hili- amshauri mzazi kuhusu uzazi?
Wadau hii ni sawa? Mtoto- hasa wa umri kama uliotumika katika tangazo hili- amshauri mzazi kuhusu uzazi?