Mimi ni binti wa miaka 25, nilianza mapenzi miaka kadhaa iliyopita na kaka mmoja ambae tulikuwa na tofaut ya miaka saba.
Uyo kaka nilimpenda sana kuliko neno sana lenyewe lilivyo, na sikuwahi kuwaza mwanaume yoyote zaid yake.
Kwa kufupisha stor, aftr seven yrs ya mahusiano nikiwa nimemaliza chuo bf alitafutiwa mchumba kwao (ni kama tamaduni zao kutafutiwa mwanamkr ambae familia inamjua na awe wa asili yao-mwarabu/mchanganyiko wa kiasia) .
Niliumia sana kwa sababu kwanza boyfriend hakuonyesha msimamo wowote ni kama alikuwa anajua nini kitakuja kutokea mbeleni. Nikaamua niachane nae japo nilikuwa kama chizi kwa muda.
Tatizo sasa nashindwa kumuamini mwanaume yoyote, sina imani na mapenzi ya kweli tena. Na tangu niachane na x wangu nimeshadate na wanaume wawili na wote najikuta tu nastopisha mahusiano bila sababu maalumu. Watu wangu wakaribu wananiambia nna matatizo ya kisaikolojia kutoka na situation iliyotokea kwenye mahusiano yaliyopita.
Wanajamvi especial wanawake wenzangu mshaexperience hii situation? Kama kweli ni tatizo la kisaikolojia naombeni msaada wenu kimawazo niwe sawa, sio kwamba sipendi kuwa katika mahusiano ya tena ila nakosa imani kabsaaaa mwanaume nahisi kusalitiwa tuuuuu mwisho wa siku naamua kumpotezea.
N.B: SITAFUTI BF HUMU JAMVINI, NIMESHARE TU TATIZO LANGU(nimejisikia confortable kushare na watu ambao hawanijui siwajui ) NA KUPATA MAWAZO YENU NA USHAURI.
Shukran!