Hili ni tatizo gani, Nimsaidiaje?

Hili ni tatizo gani, Nimsaidiaje?

Kideme

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2020
Posts
263
Reaction score
265
Moja kwa moja kwenye mada. Lakini niwe muwazi si mwandishi mzuri!

Ipo hivi, kijana wangu yupo A level bweni, jana amerudi analalamika amepata ugonjwa wa ajabu. Kwamba ana karibu wiki tatu sasa anashindwa kujisomea usiku kwani akishika kitabu baada ya kama saa moja au na zaidi kidogo anapata usingizi wa ajabu, ajabu kwa maana kwamba hawezi kujizuia na akilazimisha atastuka asbuhi akiwa amelala hapo hapo kwenye meza.

Baya zaidi anapoashwa hawezi kuamka kabisa. Hali hii humtokezea usiku tu mchana anakuwa kawaida tu. Mchana (jioni) anapata muda wa kutosha, hulala kuanzia saa 10.00 jioni hadi saa 1.00 usiku.

Amejaribu njia kadhaa ikiwa ni pamojà na kulala baadhi ya siku usiku kucha ili kesho yake apate nguvu haikumsaidia. Amejaribu kuacha kula chakula cha usiku, yaani akishakula chakula cha mchana hali tena hadi kesho yake asubuhi hii njia anasema imepinguza kidogo matàtizo lkn si kwa kiasi cha kuridhisha.

Naomba mwenye utambuzi, ushauri au dawa za kuondoa tatizo hili, nikiamini familia yetu hii JF ina utajiri wa wataalam wa kila fani.
 
Nampendekeza Mr. Mshana aje atoe ufafanuzi kidogo ktk masuala kama haya yuko vzr.

Karibu ndg utuelimisha.
 
Nilisoma na jamaa ka dogo huyo nazani ajaribu kubadili mazingira ya kusomea namaanisha usiku asome darasa tofauti na alilozoea afu asome kwa interval may be after 1 hour anapumzika kwa kutembea dk hata tatu au stor afu arud kusoma. Au ajaribu discussion zote zikishindwa bas kuna Satan mar rateng tiii.

Natumai atakuwa sawa.
 
Mwambie tu atumie muda Wa mchana vizuri , ajisomee mchana , ikifika saa nne usiku akalale tu .
Sawa mkuu. Lkn A level utapasua kweli bila kukaza msuli?
 
Nilisoma na jamaa ka dogo huyo nazani ajaribu kubadili mazingira ya kusomea namaanisha usiku asome darasa tofauti na alilozoea afu asome kwa interval may be after 1 hour anapumzika kwa kutembea dk hata tatu au stor afu arud kusoma. Au ajaribu discussion zote zikishindwa bas kuna Satan mar rateng tiii.
Natumai atakuwa sawa.
Ni ushauri mwema
 
Sawa mkuu. Lkn A level utapasua kweli bila kukaza msuli?
Inategemeana na combination mkuu na kichwa cha MTU tu, nakumbuka nilipokua A level kuna Jamaa Wa HGL walikua zao wanasoma mchana tu na walifaulu wotee hakuna aliyefeli
 
Huenda ameanza kunyetoka atapata tabu sana nyeto ni hatari ikikukataa masomo hayataenda.
Uchovu mara kwa mara.
Jaribu kumdadisi vizuri maana maisha ya boarding pia huwa changamoto Sana.​
 
Huenda ameanza kunyetoka atapata tabu sana nyeto ni hatari ikikukataa masomo hayataenda.
Uchovu mara kwa mara.
Jaribu kumdadisi vizuri maana maisha ya boarding pia huwa changamoto Sana.​
Shukran mkuu
 
Hili tatizo wanalo vijana wengi wa kibongo. Huwa linatokea kwa sababu wanasoma kwa kukariri na siyo kuelewa. Na mbaya zaidi huwa wanakusanya vitu wanavyotakiwa kuvisoma kwa muda mrefu na mtihani unapokaribia ndiyo wananza kuhaha kujaribu kukariri. Njia nzuri ya kuondoka na hili tatizo ni kufanya -review kila siku baada ya somo husika na kuhakikisha umelielewa (siyo kukariri) na siyo kusubiri mpaka wakati wa mtihani.
 
Sidhani kama kuna uchawi wowote mkuu, it's just the matter of understanding one's self. Nikwambie kitu ambacho kitamsaidia, kwanza watu wengi wanaamini mda wa kusoma ni usiku.

Mimi nilikuwa napenda kusoma usiku sana tatizo nilikuwa napenda sana kulala, nikishika kitabu/taftari kama ivo lisaa tu mausingizi kama yote.

Nilivyo gundua hali yangu basi nikabadili utaratibu wangu wa kusoma, nikipata mda mchana ndo nasoma kama ivo anavyopata mda wa kulala ndo autumie kusoma, anasoma katika mwendo wa kusamalaizi, ambapo usiku natumia kama nusu saa kupitia zile samali zangu.

Hapo ratiba ya siku inakuwa imeisha na nakuwa nimepata mda usiku mwingi tu wa kulala. Wakati mwingine kusoma si kukalili kwamba lazima usiku, kujitambua hali yako ndo kitu kizuri.
 
Sidhani kama kuna uchawi wowote mkuu, it's just the matter of understanding one's self. Nikwambie kitu ambacho kitamsaidia, kwanza watu wengi wanaamini mda wa kusoma ni usiku. Mimi nilikuwa napenda kusoma usiku sana tatizo nilikuwa napenda sana kulala, nikishika kitabu/taftari kama ivo lisaa tu mausingizi kama yote. Nilivyo gundua hali yangu basi nikabadili utaratibu wangu wa kusoma, nikipata mda mchana ndo nasoma kama ivo anavyopata mda wa kulala ndo autumie kusoma, anasoma katika mwendo wa kusamalaizi, ambapo usiku natumia kama nusu saa kupitia zile samali zangu. Hapo ratiba ya siku inakuwa imeisha na nakuwa nimepata mda usiku mwingi tu wa kulala. Wakati mwingine kusoma si kukalili kwamba lazima usiku, kujitambua hali yako ndo kitu kizuri.
Shukran mkuu. Hata mm siamini kwamba kuna uchawi ktk hili na ndio sifahamu pia ni tatizo gani. Lkn naamini kupita michango yenu nitajua nimshaurije kijana
 
Mpaka leo najiuliza, mtu anawezaje kusoma zaidi ya dk 15 akiwa mwenyewe bila mwl. Mimi nilishindwa tangia drs la 1. Hata nilivyofaulu ni Mungu mwenyewe anajua
 
Mpaka leo najiuliza, mtu anawezaje kusoma zaidi ya dk 15 akiwa mwenyewe bila mwl. Mimi nilishindwa tangia drs la 1. Hata nilivyofaulu ni Mungu mwenyewe anajua
Doh! Kwa hiyo mwalimu akupe mwongozo then akufundishe yote?
 
Nimezungumzia upande wangu mkuu. Maana mimi hata wenzangu hawakutaka kusoma na mimi maana nilikuwa msumbufu tu, ndani ya dk 5 nakuwa nimevuruga kila kitu
 
Back
Top Bottom