Llio 002
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,631
- 2,038
Habari wana jF,
Mimi ni kijana baada ya kukaa sana mtaani bila kazi ya kueleweka japokuwa nina kijielimu kangu kutoka college moja hapa mjini nimeamua kuja na wazo langu la biashara kwa ajili ya kulifanyia kazi?
Lengo la kuweka uzi huu hapa ni kwa ajili ya michango ya kimawazo katika kuliboresha wazo hilo ambalo mimi au hata mtu mwingine anaweza akalitumia na likamtowa sehemu moja na kumpeleka sehemu nyingine.
Wazo lenyewe:
Kuuza Mboga za majani.
Ukiliangalia kwa haraka inaweza likaonekana ni wazo flani hivi la kipuuzi sana. Pia inaweza isikuingie akili kama kweli muhitimu wa chuo anaweza kufanya hiyo biashara. Lakini ndio wazo ambalo mimi nimekaa na kuja nalo.
Mchakato utakavyokuwa:
Jinsi nitakavyokuwa nafanya ni rahisi sana nitakuwa na nunua mboga za majani then nazikatakata halafu nazipaki kwenye vikontena. Ndani ya kikontena kimoja kutakuwa na mboga ya majani iliyooshwa taya na kukatwa katwa pia kutakuwa na kitunguu ambacho tayari kimeshakatwakatwa na pia kutakuwa na tangawizi ambayo tayari imeshasagwa.
Nb: Kitunguu na tangawizi kila kimoja kitakuwa kimehifadhiwa peke yake then vinawekwa ndani ya kikontena cha mboga ya majani. Bei nita idetermine kwa kutumia method inayoitwa Cost based price.
Usambazaji:
Njia ya usambazi nitakuwa nasambaza mimi mwenyewe kwa njia ya kutembea nyumba hadi nyumba. Yaani kwa kifupi nitakuwa nachagua mtaa wa kudeal nao kwa siku hiyo. Kama itakuwa ni Mikocheni maana yake nitachaguwa kimtaa cha ndani ya Mikocheni na kuuza biashara yangu. Then kwenye kila sehemu ninayouza biashara yangu nitaacha mawasiliano kwa ajili ya kumpelekea bidhaa kama ikitokea siku akiihitaji.
Changamoto nizionazo mpaka sasa ni kutokujuwa gharama halisi za package za plastiki ni shillingi ngapi itakuwa vizuri kama ukiweka na picha pamoja na bei zake kama unazifahamu.
Udhalishaji.
Nimepanga kama ikiwezekana kwa kila ninapoingia sokoni kuuza biashara yangu natakiwa kwenda sokoni na vikontena mia moja na kumake sure vikontena vyote vinaisha ndani ya siku moja.
Nakaribisha mawazo ya kujenga na hata wale wa kukejeli pia nawakaribisha maana naamini yule anayekukejeli au kukusema ndio anakujenga.
Karibuni sana wakuu