Hili ndio CCM hawataki kuliamini, Lowassa unabii wako utatimia!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kila mara hua nasema kua CCM ni kama "VIZIWI" ,Yaani hawasikii wala hawaoni! Wanajipa matumaini ambayo hayawafikishi kokote, pumzi hakuna tena imekua ni huruma tupu.

Hua nawaambia kuna hapa Afrika vyama vya ukombozi vimekwisha, vimeshatolewa imebaki ANC ya S.Afrika na ZANU-PF ya Zimbabwe ambayo kwa sasa haina pumzi nayo. Muda wowote CCM Wanaondoka wala hili halihitaji tume huru ya uchaguzi.Chamsingi niwashauri tu waanze kuandika vitabu vya historia kwa ajili vizazi vijavyo ili waje kuwawasimulie kua waliwahihi kuipoka ushindi CUF 2015.


Juzi Mh Edward Lowassa alikazia hivyo hivyo kama nilivyokua nikiishauri CCM, pengine naye alisoma post zangu humu! Yaani huu unaweza kuna ni unabii tisha wa Lowassa kwenda kutimia muda si mrefu, pia unaweza usiwe unabii lkwa sababu wengi tulishaliona hili kitambo kwahiyo ni bora CCM waache kufanya siasa za kukomoana kwa kutambua kua kesho yao haiko mbali.


Hapa simaanishi UKAWA pekee ndiyo watakatotimiza hili bali ni hata wapinzani wengine ndio watakaoweza kumalizia kazi, CCM watambue watakaowatoa sio Chadema tu kwa jinsi walivyowageuza kua maadui bali ni upinzani kwa ujumla wake.


CCM ya leo ambayo itikadi zake zinaenezwa na kina Humphrey Pole pole ambaye sijui hata siasa amezijulia umri gani, sina uhakika na mapishi za propaganda za Polepooe kama zinaweza kuisogeza CCM. Siasa sio kujenga ghorafa wala madaraja au kununua ndege bali ni ufundi wa kuwashawishi watu watambue kile unachokifanya.
 
CCM ilisha ondoka 2015 lakini nguvu ya dola, tume na siasa za upole za baadhi ya viongozi wa upinzani ndiyo ikawa pona yao.
Hayo sidhani kama yatakuwepo tena 2020. Na watakao shinikiza kwa kutumia nguvu bila kuwaonea huruma sio wale wapinzani walio kuwepo siku nyingi bali hawa wanaotoka ndani ya ccm kwa madhila makubwa ikiwapo uonevu
 
CCM ilisha ondoka 2015 lakini nguvu ya dola, tume na siasa za upole za baadhi ya viongozi wa upinzani ndiyo ikawa pona yao.
Hayo sidhani kama yatakuwepo tena 2020. Na watakao shinikiza kwa kutumia nguvu bila kuwaonea huruma sio wale wapinzani walio kuwepo siku nyingi bali hawa wanaotoka ndani ya ccm kwa madhila makubwa ikiwapo uonevu
True !
 
Itaondoka kwa upinzani gani? Labda wajukuu wetu ukooo mbeleni wawe serious lakini kwa sasa nikujilisha upepo tu.
 
66700b9324e4b675931ca74812d1bd79.jpg
Siku moja itakuwa. Kazana Eddo kazana. Hakuna kukata tamaa!
 
Tanzania hii tunahtaji maombi hili kuiondoa CCM, wajinga wengi...
Ni kweli Mkuu, tena wajinga wakubwa ni wale wanaojipambanua kuwa ni wapinzani wanaitaka kuiondoa Ccm madarakani. Kwa miaka yote hii wameshindwa kusoma mchezo, hawana forward wazuri wala mabeki, daily visingizio visivyo na vichwa wala migumu pasi na kujipanga.

Ni aibu sana kwa chama kijionacho kuwa ndicho kikubwa ktk upinzani kuwa na sera matukio. Hakieleweki, hakishauriki, hakijifunzi, hakijisawazishi, ni laana hii.

Ni jambo la kihistoria, kuzaliwa na kufa. Ila kwa mikakati hii, vingine vitasubiri sana au vitafanikiwa lakini kwa muhula mmoja tu na Ccm zitarudi tena na hadithi itahairishiwa hapo kwa miaka mingine 50.

Nilitaraji upinzani ungefanya hata kwa uchache tu yale ambayo wanawatakia wananchi. Kupitia utajiri wa viongozi, ruzuku chache, hata kwa kuwapa semina bora vijiji na kata wanazozimiliki ziwe ni tofauti na za ccm, lakini wapi?

Leo upinzani ndo washindani hata kwa yaliyo bayana kama maswala ya elimu, afya miundombinu nk, watz wa kumsikiliza pumba hizi hawapo.

Tz na watz wa kawaida, hawa hitaji cha demokrasia wala kulitazama bunge, wanataka huduma bora, uwajibikaji, kuheshimiwa ofisini, kukomeshwa kwa yule aliye semekana ndo adui wao "ufisadi." tu basi. Ukipingana na haya, haya endelea kuota.
 
mene mene tekeli na peresi
Utaanguka but truth me sio kwa miaka ya karibuni, upinzani huu wa sasa umejaa uhuni tu leo useme hivi kesho unageuza maneno yake hivi nani atakayewaamini hahaha tunahitaji upinzani unaojielewa, upinzani wenye nguvu, upinzani wenye hoja zilizoshiba, sio wenye hoja nyepesi nyepesi zizisokua na mashiko.
 
Ni kweli kuwa CCM itaondoka lakini usitarajie chaggadomo au hii nchi kuangukia mikononi mwa mamangi. Majizi na mabadhilifu hayawezi kupewa nchi hii
Hoja kama hizi cdm ingekuwa na malengo thabiti wangeshazitafutia muafaka wake, kimya na itakuwa hivyo hadi 2020 na zitawatafuna na kutaka kusema wameibiwa tena kura, hawa ni vilaza sana niko na mashaka na vyeti na elimu zao.

Mbona siasa ni simpo game, wsnadhindwaje? Hawana nia ya dhati hawa wapiga dili. ZZK naye anajiharibia wakati ndiye tuliyemdhania kuwa mkweli.
 
Hoja kama hizi cdm ingekuwa na malengo thabiti wangeshazitafutia muafaka wake, kimya na itakuwa hivyo hadi 2020 na zitawatafuna na kutaka kuibiwa tena kura, hawa ni vilaza sana niko na mashaka na vyeti na elimu zao.

Mbona siasa ni simpo game, wsnadhindwaje? Hawana nia ya dhati hawa wapiga dili. ZZK naye anajiharibia wakati ndiye tuliyemdhania kuwa mkweli.
Tatizo ni uwepo wa malengo yanayotofautiana ndani ya chama.

- Wakati wengine wanafikiria ni chama cha kupigania maslahi ya watu


- Wenye chama wenyewe ( Mtei & Mbowe ) wanajenga CHADEMA kama kampuni binafsi ya kujiingizia kipato.

Kwa mantiki hiyo usitegemee watafika popote
 
Mmh! Unazungumzia ccm kuondoka madarakan ili hali hivyo vyama vya upinzan havina hata ofic mikoan
 
Mmh! Unazungumzia ccm kuondoka madarakan ili hali hivyo vyama vya upinzan havina hata ofic mikoan
Hivi hata hili la watanzania wengi kuishi vijijini hawalijui kweli? Wana kata zinazoongozwa na cdm, lakini hata siku moja husikii chama kukufanya lolote lile kuwapita tafu hawa hata kwa mawazo tu ili kata zao ziakisi wanachokihubiri, nyingi hata maendeleo zinakufa haswa mbunge akiwa ni wa ccm na pakitokea mbunge muuaji wa siasa kuwasaidia madiwani, na wengi 2020 watagombea kupitia ccm.

Hawana mikakati, hawashauriki, wajuaji, vilaza, wabinafsi. Hakuna wa kuwapa nchi ktk mtindo huu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom