CCM acheni CHADEMA wamtumie LOWASSA, acheni kulialia

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Kama kuna kitu kinawaumiza CCM Kwa sasa ni kuwepo kwa mawaziri wakuu wastaafu ndani ya upinzani, hawa wana siri nyingi sana za CCM na serikali yake, wanaweza kucheza nayo watakavyo, wanaweza kuwapa upinzani siri zote za CCM na hali halisi ilivyo.

Mtu kama Lowassa amekua mjumbe wa halmashairi kuu ya CCM muda mrefu, Lowassa amekua kiongozi wa UVCCM muda mrefu enzi za ujana wake! Huyu anazo siri zote za CCM kuliko pengine hata mwenyekiti wa sasa wa CCM na hili halina ubishi kabisa.

Lowassa alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kucheza na chama cha mapinduzi na kulifanya jina lake kua kubwa ndani ya chama kabla ya kuhamia CHADEMA kwa sababu alikua akikifahamu chama hicho vizuri.

Watu kama kina TINDU LISSU wako karibu sana na Mh Lowassa hatujui wanapewa ima wanafunzwa kitu gani kuhusu siasa za CCM na serikali yake, hapa ndipo ambapo unaweza kusema CHADEMA wananufaika nao sana ndio maana CCM bado wanaumizwa sana na uwepo wa watu hawa ndani ya CHADEMA.

Sijimzungumzia Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mzee Apson Mwang'onda ambao walikua watu muhimu sana katika serikali zilizopita, na nina uhakika kua wazee hawa kuna vitu wanawamezesha vijana wa CHADEMA mpaka hivi sasa, Japo kwa kazi kama za Mzee Mwang'onda sheria za nchi zinamzuia kiusema chochote juu ya mambo yanayohusu usalama wa nchi yetu lakini hakuna anayejua kua muda wote anafanya nini na yuko wapi.

Lazima tukubali kua kupitia wakongwe hawa wa siasa za Tanzania kua ndani ya upinzani kunaongezea sifa za kutosha juu ya Upinzani kuongoza taifa, kupitia hili suala hata kwa wale wanaodhani kua upinzani unaweza kufa badala ya kustawi zaidi wanajidanganya na kujipa matumsini hewa.

Kwa hisia zangu ni kwamba, Wanasiasa kama kina Tundu Lissu na Lema sio wana misimano yao binafsi bali kuna vitu wamekwisha funzwa na ndio maana hawataki kabisa kuzibwa midomo. Tundu Lissu nimjuavyo mimi ni aina ya mwanasiasa mjanja sana, hawezi kua kukaa karibu na Mh Lowassa au Mzee Kingunge bure! Kuna kitu anafunzwa kuhusu taifa hili.
 
Hivyo, ushauri wa kipekee kwa CHADEMA ni kuwapuuza CCM na lelele zao,watulie mzee awape nondo za kutosha.
 
Nyumbu badala ya kukomaa na kauli za ccm, ni bora mkakomaa kutimiza ahadi zenu kwa wananchi.

Mliahidi Arusha ikiwa chini ya chadema itapaa kimaendeleo kama ulaya, lkn mpaka sasa mwaka umeisha hamna chochote ni porojo tu.

Je mwaka 2020 mtatudanganya na nini wananchi Wa Arusha??
 
Wewe ndio unatakiwa ujiulize kua 2020 CCM itawadanganya nini Watanzani na ulaji wa pesa za Kagera? Million 50 kwa kila kijiji ziko wapi? Mpaka sasa kuna viwanda vingapi? Tulieni 2020 siobali, watanzania wamechoshwa na ntalalila.
 
Mwlm aliwahi kusema upinzani wa kweli unataka ndani ya CCM ndo maana mapovu kedekede yanawatoka wakimwona au kusikia eddo
 
Nyumbu badala ya kukomaa na kauli za ccm, ni bora mkakomaa kutimiza ahadi zenu kwa wananchi.

Mliahidi Arusha ikiwa chini ya chadema itapaa kimaendeleo kama ulaya, lkn mpaka sasa mwaka umeisha hamna chochote ni porojo tu.

Je mwaka 2020 mtatudanganya na nini wananchi Wa Arusha??
Sisi tuwape pesa ili tuje tuwakamate vzr vinginevyo watakuja jitetea hapo mbeleni tutashindwa kuwakamata.
 
Back
Top Bottom