MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,255
- 8,027
Kama kuna jambo ambalo watu hawalifahamu kuhusu Lowassa ni maandalizi yake na mbio za urais tokea mwaka 1995, Huyu mtu ana mtandao mkubwa nchi nzima bara na visiwani! Hana wasiwasi na safari yake ndio maana anatupiwa matusi ya kila aina na wala hana muda wa kuyajibu maana anajua vijimambo tu vya mtaani vya kupuuzia tu.Maandalizi yake ni ya muda mrefu sana kuliko mgombea yeyote yule ndani ya vyama vyote!
Shida pamoja na wasiwasi wa LOWASSA ulikua kwa ile kamati mkuu ya CCM iliyojaa chuki na unyanyapaa mkubwa,ila kwa upande wa wananchi anajua kua wanamfahamu vizuri na hana wasiwasi nao na ndio maana kwa upande wa CHADEMA ambapo hakuna chuki wala unyanyapaa kwa sasa anatanua na wala hakuna wa kumzuia kushinda urais.
Magufuli hakua amejiandaa kabisa na safari hii hali inayowapa wakati mgumu CCM mpaka kutumia misuli mikubwa kumuuza, hakua na mtandao mahali popote wa kumpa tafu ya ushindi, hakutegemea kabisa kua angekabidhiwa kijiti hiki na chama chake ambacho kinaonekana kumpwaya Kwa mbali kabisa!Achilia mbali mitandao ya watu ila katika mitandao ya kijamii Sijui ni mtandao upi wa naweza kumkuta Magufuli kati ya Fb,twitter,Instagram au mingineyo!
Sasa jiulize kama mgombea urais hakua na account hata moja kati ya mitandao tajwa hapo unategemea nini hapo? Kama yupo basi nafikiri ni baada ya kukabidhiwa kijiti cha urais na chama chake.Sina uhakika kabisa kama upande wa Zanzibar Magufuli anaweza kua na jina kabisa kumfananisha na LOWASSA.
Naiona tofauti kubwa kabisa ya umaarufu wa hawa watu wawili! Si kazi rahisi kwa Magufuli kuuza jina lake pande zote za jamhuri ya muungano kama ambavyo LOWASSA alikwishafanya siku nyingi, kwa upande wa Zanzibar watu wanaifahamu CCM tu na sio Magufuli ambaye alikua waziri wa ujenzi bara. Kwa hapa ndiko iliko tofauti ya watu hawa wawili.