Hili liwe funzo kwa polisi wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili liwe funzo kwa polisi wote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwinukai, Sep 13, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  "AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO" Huu ni ujumbe kwa askari polisi wote, kutokana na utii wao wa amri sasa wameanza kutumika vibaya, kama kuua raia bila kujua kwamba watoa amri hizo hawatakuwanoa milele na vile vile pia nao wanamipaka ya kuwatetea.kama hili la IRINGA
   
 2. N

  Nguto JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,650
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  At the end of the day wewe ulieua ndie unasimama kizimbani kujibu shtaka la kuua. Lazima kufikiria mara mbili amri unayopewa wewe askari!! Kijana wa watu miaka 23 keshajiharibia maisha hata kama watamtetea asifanywe kitu. Damu ya Mwangosi itaendelea kumlilia hadi yeye atakapoingia kaburini.
   
 3. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,949
  Likes Received: 6,706
  Trophy Points: 280
  Kitu cha msingi hapa ni polisi kutumia akili za mbayuwayu (za kuambiwa na zao wenyewe) maana hilo tukio la Iringa, ingawa ushahidi wa mazingira unaonyesha wazi kuwa yule askari alipewa maelekezo na Kamuhanda, kufanya aliyoyafanya kwa Mwangosi, lakini tunaona ni yeye, peke yake ameburuzwa mahakamani, na wale waliomtuma,akina Kamuhanda, wanapeta uraiani!!
   
 4. n

  nkikiki Senior Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Amri za wakubwa jeshini zifanyiwe marejeo ili zisisimame kama pai! kama agizo la ua na afande anaua kweli.
   
 5. k

  kygrykos Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwache ile upande wake huyo kilaza. na bado wale waliofanya mambo kama hayo mikoa mingine. wanadhani hao waliowatuma watakua kwenye madaraka milele.ipo siku watakuja kupatikana wote waliowanea wananchi. ajitete mwenyewe sasa. waliomtuma kuua wamemwacha, yey ndo katolewa kafara.
   
 6. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni fundisho tosha kwa askari Polisi
   
 7. M

  MTK JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Polisi wajenge utamaduni wa kujisomea somea na kubwa zaidi wasome General Police orders (GPO) ambayo ndio operating manual ya kazi zao; waache kufanya kazi kwa mazoea tu au kupokea amri kama robots.
   
 8. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee babaangu imekula kwake polisi alie uwa!!! Mi nashanga sana hawa polisi wetu si kila ki2 unachoambiwa lazima utekeleze chuja kwanza kabla ujatekeleza kwani ukiambiwa ule mavi utakula ????
   
 9. K

  Kanansi New Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kwamba polisi watafakari faida na madhara ya kutekeleza amri wanapopewa amri na wakubwa zao. Kama mtuhumiwa wa mauaji ya Mwangosi, hivi hakujua kuwa kuua ni kosa la jinai kisheria? Mauaji anayotuhumiwa nayo yalikuwa na tija gani kwake. Polisi changanyeni na zenu, kumbukeni kwamba nyie ni sehemu ya jamii na wala hamko juu ya sheria.
   
 10. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wana amri yao isemayo 'tekeleza kwanza kisha mambo mengine baadaye' na nadhani itakuwa inakinzana na hii ya 'changanya na zako'
   
 11. N

  Nguto JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,650
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  He respected the order and he thought he would get away with it!!! Polisi lazima mtafakari mara mbili mbili hizo amri mnazopewa na wakubwa zenu. Someni sheria za nchi hii mzijue na pia muwe watu wa kutenda haki. Msituonee kwa vile mko kazini wakati kesho mtakapostaafu mtakuja kwetu. Mkija mnadhani tutawapokea wakati mnatuua? Tutawambieni muende kwa wakubwa zenu waliowambia mtuue mkaishi huko!! Polisi mnatakiwa mtulinde sisi na mali zetu sio mtuue!! Hivi huwa wanasoma hizi post?
   
Loading...