Hili linasababishwa na nini?limekuwa Sugu sasa kwa Watu wengi

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Mtu anakupigia simu au anakutumia text, baada ya salam unamuuliza nani mwenzangu? kwa ustaarabu kabisa. majibu yake sasa ndo utakoma
1. inamaana ume delete namba yangu?:(
2. ina maana umesahau sauti yangu?(huku amekunja sura):confused:
3. Otea atakuwa nani? (huku anatabasamu huko aliko)
4. Kama ni hivyo basi, na kama ntakupigia tena siyo mimi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ( anakata huku amekunja uso):confused:
5. Ndo nakupa homework nitafute mpaka ujue mi nani...anakata simu ( unajenga picha huko aliko huyo mtu anatabasamu kipuuzi kabisa):)
6. Mi demu wako umpendaye sana ( huku anatabasamu huko aliko):)
7. Mi mchepuko wako bwana umenisahau( huku anajichekesha kifedhuri):D
8. Mi ni Mwanakombo ( kuna akina mwanakombo wangapi duniani? malizia jina lote na maelezo kidogo k.m tulisoma wote Mchambawima Primary School):rolleyes:

tubadiliken wapendwa simu huwa zinaharibika,zinapotea,zinaibwa n.k mi siwez kuwa na kazi ya kukariri sauti za watu nipo busy. ukiulizwa nani mwenzangu jibu tu kirahisi mimi ni mwanakombo ndendeule tulisoma wote shule ya msingi mchambawima darasa la 5 B kabla hujahamishiwa C. au mimi nilikutana nawe club usiku ulikuwa bwii...tukatoka nje gizani tuka..ukasema umependa tugawane namba za simu ndo leo nimeona nikusalimie...
 
Walio wengi ni kukosa exposure na kudhani kuwa wewe umegeuka kuwa KANZI DATA MAKUMBUSHO YA TAIFA
ya kutunza taarifa zake . Kumbe na wewe una mambo mengi mia kidogo.
 
mimi kama ukinitafuta na Number ngeni hata sikuulizi wewe ni nani. utaongea shida yako. ntakujibu kutokana ma mazungumzo yako.
na SMS ukituma nakujibu tu kama kawaida. maana nilishawahi tukanwa na mtu simfahamu wala hanifahamu ziidi ya kukosea tu. number. anakuja gundua. kanitukana mpaka basi. nikakoma
 
Mtu anakupigia simu au anakutumia text, baada ya salam unamuuliza nani mwenzangu? kwa ustaarabu kabisa. majibu yake sasa ndo utakoma
1. inamaana ume delete namba yangu?:(
2. ina maana umesahau sauti yangu?(huku amekunja sura):confused:
3. Otea atakuwa nani? (huku anatabasamu huko aliko)
4. Kama ni hivyo basi, na kama ntakupigia tena siyo mimi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ( anakata huku amekunja uso):confused:
5. Ndo nakupa homework nitafute mpaka ujue mi nani...anakata simu ( unajenga picha huko aliko huyo mtu anatabasamu kipuuzi kabisa):)
6. Mi demu wako umpendaye sana ( huku anatabasamu huko aliko):)
7. Mi mchepuko wako bwana umenisahau( huku anajichekesha kifedhuri):D
8. Mi ni Mwanakombo ( kuna akina mwanakombo wangapi duniani? malizia jina lote na maelezo kidogo k.m tulisoma wote Mchambawima Primary School):rolleyes:

tubadiliken wapendwa simu huwa zinaharibika,zinapotea,zinaibwa n.k mi siwez kuwa na kazi ya kukariri sauti za watu nipo busy. ukiulizwa nani mwenzangu jibu tu kirahisi mimi ni mwanakombo ndendeule tulisoma wote shule ya msingi mchambawima darasa la 5 B kabla hujahamishiwa C. au mimi nilikutana nawe club usiku ulikuwa bwii...tukatoka nje gizani tuka..ukasema umependa tugawane namba za simu ndo leo nimeona nikusalimie...
Alafu akikata simu utasikia jamaa anadharau kweli tangu ashike pesa sio mwenzetu
Wajinga bhana
 
Hawa watu wanazidi kuongezeka wapuuzi sana. wanaamini wewe siku zote kazi yako ni kukariri namba zao au sauti zao. ukiuliza kweli wanaanza kukuchimba kuwa una majidai n.k kumbe simu hupotea pia na wakati mwingine hata kuibwa. kistaarabu mtu anapaswa ajitambulishe tu mi flan.

Hilo ndo la maana ila chunguza kitu kimoja wenye tabia hizo wote na wenye majibu hayo wanakua wamepiga simu awana la maana ivi unazani mtu mwenye shida na wewe kabisa ya muhimu awezi kuja na ujinga huo ni wakuwapuuza tu
 
naona umetaja jina la shule uliyosoma
shule ya msingi mchambawima
 
sasa utasikaje wakati tayari keshakata simu?
Fanya akili yako kuwa nyepesi tunaongelea,uyo mtu ukimkatia simu uko aliko anaanza kuwaambia watu aliokuwa nao maneno kama hayo mnataka tuandike kama tunawaandikia wale wanao jua kusoma na kuandika
 
wewe umesema utasikia akisema, hilo neno "huko aliko" umeliongezea sasa
 
wanaboa kwakweli mimi huwa niko direct kama hauko tayari kujitambulisha basi uwe na siku njema sijibu tena simu wala sms. ila wanaoboa zaidi ni wale ambao unakuta missed call ya namba ngeni kwenye simu yako unachukua uamuzi wa kumpigia simu anapokea unamuuliza vizuri "nani mwenzangu umenipigia nimeona missed call ya namba ngeni" halafu anakujibu na sauti kali "kwani we nani,unamtaka nani?" hawa huwa wanaboa jamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom