Hili limeshakuwa tatizo: Dola sasa ni zaidi ya TZS 2,350/= Kikwete, Ndulu, Wizara wapo kimya!

Mh.Rais Kikwete mimi na watanzania wote ambao tuna elimu ya kufuatilia na kuyajua mambo haya ya uchumi tunakuomba chondechonde ingilia kati anguko hili la sarafu ya Tanzania,tunajua wewe kitaaluma ni mchumi tuna imani wewe na wataalamu wenzako serikalini mna uwezo wa kuigeuza hali hii isizidi kutuumiza.
 
Ni kweli unachosema, hii ada nalipa kwa Italy sio hapa Tanzania. Hakuna jinsi

Tatizo ndio linaanzia hapo ... unless unalipa ADA nje ya nchi hakuna sababu ya kutumia dollar. Tatizo kubwa la nje hizi zinazoendelea zisizo na viwanda na zinazotegemea kuagiza mpaka toothpick ndilo hili.. tungekuwa tunajitemea kwa mahitaji mengi wala tusingejali dollar ikipanda.. Nchi kama China zinashusha hata thamani yao kwa makusudi against the dollar sababu inakuwa rahisi kwa watu kununua kwao (things became cheaper)

By the way sio kwamba Tshs imeshuka tu.... Bali Dollar imepanda against most currencies..., ushauri kama unanunua vitu nje jaribu kuangalia alternative currencies kama ni China cheki Chiniese Yuan
 
friend we are not talking about the trend but the speed of depreciation. Kenyan shilling inspite of the attacks has only depreciated by 4 Kenyan shillings (80 Tanzania shilling) since the start of the year and not 180 shillings ( approx. 9 kes).
 
Tunaotumia za madafu tunajionea sawa tu.Pole mdau
Kiongozi hujui ulisemalo. Kushuka kwa thamani ya shilingi kwa namna fulani huchangia mfumuko wa bei. Kwa maana hiyo hata ww utaumia utake usitake. Kwa nchi nyingi za kiafrika na hasa kusini mwa jangwa la Sahara unapokaribia uchaguzi fedha za ndani hushuka thamani. Mosi ni kwa sababu chaguzi nyingi sio za kidemokrasia, kwa maana hiyo watu wengi wenye uwezo ki uchumi huamua kuzibadili fedha zao kutoka Tsh kuwa $-dollars. Pili viongozi wengi wa umma hujiingiza kwenye vitendo vya kifisadi kwa lengo la kupata hela za kununua wapiga kula. Pesa hizi huongeza "ujazo" wa fedha usioendana na uhalisia wa uchumi ktk mzunguko wa fedha. Kwa kipindi chote kuelekea uchaguzi mkuu uwekezaji husuasua sbb ya joto la uchaguzi kwa maana mpaka sasa uchaguzi ujao hautabiliki ama waliopo wataendelea au walioondoka kwenye Bunge la katiba wanaweza kuingia. Lakini hata waliopo wakiendelea atakae ingia bado ni kizungumkuti. Tatu tumekuwa tegemezi sana kwa bidhaa za nje pasipo kuwa na mikakati ya maana ya sisi kuuza nje, kwa maana hiyo uhitaji wa fedha za kigeni unakuwa mkubwa.
 
Daah mkuu mbona unatutisha aisee!!!

Nisamehe bure siwatishi bali hiyo ni realistic approach! najua wengi wetu tanapenda kusikia tunachopenda; lakini ukweli kuhusu uchumi wa nchi hii ndio huo unfortunately!! Nchi kwa sasa inategemea service industry; kuuza vocha; Mpesa; kuagiza bidhaa nje na kusambaza; hatuzalishi bali tunaagiza kwa pesa za kigeni kutoka nje na kulanguana hapa nyumbani; kwa hiyo demand ya FX iko juu wakati supply ya fx iko chini kwa sababu hatuexport kuingiza fx ambayo ingekua counter measure ya downward spiral ya shilingi yetu!! viwanda vinavyofanya kazi vizuri ni kama Tanzania breweries na vile vya cement ambavyo almost kila kinachozalishwa ni for local consumption! forex itatoka wapi ku-stabilize demand na supply ratio?!

Lakini Dont loose hope; may be a better tommorow is on the horizon!!
 
tatizo CCM.chama hovyo .sekta zote wapo makada wao wanavyeti vya kufoji.bot watoto wa viongozi wa ccm wameja na vyeti vya kufoji.we unategemea wataweza kudili na uchumi.
 
friend we are not talking about the trend but the speed of depreciation. Kenyan shilling inspite of the attacks has only depreciated by 4 Kenyan shillings (80 Tanzania shilling) since the start of the year and not 180 shillings ( approx. 9 kes).

My Point Is......., Kama tutaendelea kuwa Taifa la Wanunuzi na sio Wauzaji, tutaendelea kulia na kutegemea /kuendeshwa na fluctuations ya Currency za wenzetu, ila tukiwa at least tunajitegemea kwa mahitaji mengi iwezekenavyo fluctuation ya currency za wenzetu hazitatusumbua, (hio ni hatua ya kwanza..) Hatua ya pili tukiweza kuzalisha / kuwa na product au services ambazo wenzetu wanazitaka huenda hata kushuka kwa currency yetu ikawa ni blessing sababu ukilinganisha na wenzetu wanaouza product hizo hizo zetu zikaonekana ni bei rahisi....

Hence the only permanent way ni self reliance na uzalishaji tubadilike kutoka kuwa taifa la wanunuzi... Kuna products kibao ambazo hakuna umuhimu wa kuziagiza.., to name just a few:-
  1. Karatasi
  2. Furniture
  3. Vyakula mfano Matunda
  4. Dairy Products n.k.
Hata Dawa kama tukijikita kwenye kuboresha na utafiti wa mitishamba hakuna sababu ya kutumia pesa nyingi kuagiza dawa...

Kwahio unless the above is done...., tutaendelea kupiga hizi ngonjera until Kingdom Come.....
 
hivi tatizo nini hasa kinachopaisha hii dola kiasi hiki?? ni impact ya zile hela za wafadhili walizogoma kutoa?
Ni hali ya sintofahamu iliopo sasa :shocked::shocked:. Nyie mnaosema mnatumia pesa za madafu, mtakujakuta bei inapanda juu, wewe subiri. Ilitakiwa uchumi ukue hasa ukizingatia factor muhimu mafuta yameshuka bei lakini kinyume chake bei zitapanda ndio mana kumekuwa na kigugumizi katika kushusha nauli za mabasi.
 
Itaendelea kushuka tu kwasababu hatuzalishi na kuuza nje bali tunaingiza bidhaa karibia zote kutoka nje na sisi tumebaki kuwa omba omba. Zaidi ya nusu ya bajeti ya nchi inategemea wahisani. Wakigoma kama walivyofanya kutokana na wizi wa Escrow ndivyo hali inavyotegemewa kuwa. Kunapokuwa na ufisadi na wizi mkubwa wa fedha za umma sio ajabu thamani ya shilingi kushuka. Hatuwezi kudhibiti thamani ya pesa yetu wakati hatuna cha kuuza nje
 
safi sana. kweli wewe ni mfano wa mungu sio majitu mengine humu ambayo yanataka kulibadili jina la jamvi liwe "the home of great foolers"
 
Tuombe vita vije vivunje misingi mibovu ya serikali ya ssm

Una uhakika vita ndio suruhisho, nipe mfano hai kwa nyakati hizi wapi vita ilisaidia.
Njia sahihi ni kubadilisha uongozi kwa njia ya kura. Hata kama wataiba kura lakini tukiwashinda kwa kura za SUNAMI hawataweza iba kura zote. Tunatakiwa kushinda kwa asilimia 80% hapo wataiba mpaka wachanganyikiwe lakini ushindi utapatikana. Hii inawezekana endapo kila mtu hususani wale wanaosema, hata wakipiga wasipige fulani atashinda. Uchaguzi uliopita wengi wasiopiga walikuwa wa style hiyo.
 
There ia no hope. We can shout as much as we can. They dont care. Even at 2500. There is no hope. The president does not care. Beno does not care and the MoF doea not care. CCM does not care.

We are dealing with incompeteny economists at BoT and the MoF.
 
si wajazie tu ifike 2000 bila chengi ili tuanza kuzoea kama wabunge walivyopandisha bia kutoka 1500 mpaka 2300, tukawaomba mameneja wauze 2500 kwa baa za kinondoni na sinza hili miambili iache kutoboa mifuko yetu. Siku hizi ni kupandisha kwa kwenda mbele hadi kitimoto kimetoka 8,000/= hadi elf 12,000/= na hakina ushuru.

Hahahahahahahaha, umenena vyema mkuu
 
Tunaotumia za madafu tunajionea sawa tu.Pole mdau
Hahahaaa mkorosho bana.maumivu yatakufikia tu mbona!kwanza mafuta ya kuendeshea magari yatapanda kwasababu yananunuliwa na dola,pia nguo nazo huagizwan.k.Hilo bado unalo mtu wangu wala hujavuka mto.
Kiukweli hali ni mbaya sana.mie nilitaka kuagiza kitu fulani toka nje ila baada ya kuona the lowest 1 Usd =1927 Tsh nimepigwa na butwaa nisijue nikimbilie wapi.
 
Mlishaambiwa za madafu sasa mnategemea nini? Kuna waliojitutumua na kujibana kupeleka watoto international hadi kizunguzungu tunapata.
Haijalishi tunafanya kazi kiasi gani, tunachakarika kiasi gani mwisho mfumo unatuangusha. Mwaka jana spet mtoto kaanza ahule kwa rate ya 1500 mwaka huu, juu la ongezeko la kawaida la mwaka ada imepanda eobo tatu!!!!
Ndio hapo tunaanza hadi kuingia kwenye biashara za kukodisha mikokoteni. Middle class zinapigania resources na low class.
Walahi patachimbika karibuni.
 
Unalala kesho hauna uhaki nayo. unaweza hata kuta 2000...

Back
Top Bottom