Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,844
- 43,317
Wasalaam wana jamvi.
Wanajamvi jana kwenye taarifa ya habari ITV tulishuhudia Kamanda Sirro akieleza kuwashikilia watuhumiwa wa wizi wa mafuta ya ndege za ATCL tena wakiwemo maaskari, wengi wanaweza kufikiri kuwa huu ni wizi wa kawaida ambao watu hufanya kwa kuiba mafuta ya ndege na tena wengi wamezoea...
Lakini kama mtu alipata wasaha wa kumsikiliza kamanda Sirro atagundua kuwa huu ni uhujumu dhidi ya ndege za ATCL na Sirro alieleza hatari inayoweza kutokea kama jambo hili wasingelibaini na kuwakamata maana walikokuwa wanakwenda ni kuhatarisha maisha ya abiria wa ATCL.
Tangu zinunuliwe ndege za Bombadia wengi wamekuwa wakizipinga na wengine walikwenda mbali zaidi kusema ni mitumba na wengine wakasema hazina break na mambo mengi kwa hiyo ni ukweli ulio wazi maadui wa ndege hizi ni wengi sana na wapo na watafurahi sana likitokea jambo la kukwamisha ATCL na hawashindwi kushirikiana na watu kuhujumu ndege hizo maana ni furaha yao ndege hizo zikishindwa kuruka hili tuu kuthibitisha maneno yao.
Ni wito kwa Mamlaka husika kuanzia kwa Sirro kufanya uchunguzi wa kina kwenye jambo hili kwani wahusika sidhani kama lengo lao ni moja tuuu lazima muhakikishe mnabaini na kujiridhisha kama hakuna msukumo wa watu kwenye uhujumu huu lazima wabanwe vyema ili wathibitishe kuwa hakuna msukumo.
Nina imani kabisa vyombo vyetu vya usalama vitalichunguza sana jambo hili kupata ukweli zaidi na lengo la wizi wa mafuta yale.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Rais John Pombe Magufuli.
Wasalaam...........