Hili la Waziri husika kuhoji Yanga Kupeleka kikosi B Dodoma ni Sawa??

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,675
Nimejaribu kuperuzi habari mbalimbali za michezo nje na ndani ya nchi kubwa nililokutana nalo ni hili la Waziri husika Kuhoji uhalali wa Yanga kupeleka kikosi B kucheza na Kombani ya Majeshi Dodoma na kutoka sare ya 1-1 kikosi B cha Yanga kipo chini ya kocha Shedrack Nsajigwa.

Ukiangalia Kikosi cha wakubwa cha Yanga kinamichezo migumu&muhimu sana na pia wachezaji wengi muhimu walikua majeruhi,Sijui labda kama ni makubaliano yalifikiwa na upande mmoja ukavunja makubaliano hayo hapo sawa sheria ichukue mkono wake ila kama Kulikua hakuna makubaliano sidhani kama kuna haja ya kulichukulia hili suala siriazi kihivyo.

Sio mbaya tukitoa sapoti kwa Timu zetu za Vijana nao wapate michezo kadhaa ya kujiweka sawa,na pia timu inapopata majeruhi klabu ndio huingia gharama za matibabu kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Je wewe mdau wa mpira unasemaje juu ya hili?
 
Jana waziri Mwakyembe alilazimika kutoka uwanjani ( Jamhuri stadium Dodoma ) kwa hasira kisa YANGA wamepeleka uwanjani kikosi cha pili ili kucheza mechi ya kirafiki na kimbaini ya timu ya vikosi vya ulinzi,ameongea maneno mengi kwa hasira hadi watu wanashangaa na akasahau kuwa yanga inakabiliwa na mashindano makubwa ikiwemo jumapili dhidi ya mbao fc.
 
Huyu Mzee amekua kero timu yetu bado Ina mechi ngumu tena za muhimu kwa timu yeye hilo halioni anajua kulalamika tu
 
Hivi sakata ripoti ya nape kuhusu uvamizi wa clouds , ishu ya Roma na juzi uvamizi wa mungiki wa lipumbavu amevifukia au kasahau au ndio kusema haelewi kinachoendelea kuna nn nyuma ya pazia?
 
Hayo maneno ulimsikia akiyasema au umeyasikilizia wapi?
Sijabuni hii taarifa kwa hiyo unakata sasa au?jaribu kufuatilia vyombo vya habari vya michezo mfano salehe jembe na wengineo utapata habari zaidi.
 
Back
Top Bottom