samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 217
Mi naona sawa tu maana hivi Bar zimejaa kila kona ya nchi mpaka kwenye sehemu za kuishi watu, utakuta mtu anafungua Bar karibu ya shule, Kanisa na Msiki. Hii Tabia inazidikukuwa maana hakuna serikali inayofuata sheria ufisadi kila kona. Yanahitajika mapinduzi kama ya Tunisia au Misri

Wakati kama huu ndipo huwa natamani ningekuwa mzanzibari.
Saafi sana wazanzibari endeleeni na moyo huo huo.
Tatizo siyo mabaa ambayo yako kwenye sehemu zake zinazostahiki, yaani mahotelini, beach na kadhalika. Tatizo liko kwenye mabaa yanayofunguliwa ovyo kwenye maeneo ya watu (residential areas). Nimesikia kwenye redio wananchi wamelalamika kwenye hayo mamlaka ya leseni na vinywaji without success, ndiyo maana wamechukua hatua mikononi mwao.
Baa zilikuwepo tangu enzi ya mkoloni lakini hakukuwa na nakama hii ya sasa.
Stereotype illusion...km kosa kafanya mtu mmoja sioni sababu ya uzanzibari,na km aliyefanyiwa ni John pia sina hakika km mhalifu alilenga watu wa dini fulani....wakuu tuchunge sana hukumu za kiujumla!...km kosa kafanya Rutashobya haitoshi kusema "wahaya ndivyo walivyo..." likewise kofi moja la bwana Mwita halitoshi kusema " Wakurya ndivyo walivyo"...tuchunge sana kauli hizi!
nashangaa,wanakusanya kodi kwenye hotel zinazouza bia!waache unafki hao wazanzibari mbona hawachomi moto hoteli za kitalii zinazouza pombe na nyama ya nguruwe pia? Au uadui wao upo kwa wazanzibari/wabara wenzao wenye mabaa?