Konda wa bodaboda
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,981
- 4,169
Jana kuna mada iliwekwa hapa jf kuhusu Lukuvi kukataa hongo ya bilioni 5 kutoka kwa wawekezaji waliotaka kuiuzia serikali ardhi kwa shilingi milioni mia moja na zaidi kwa ekari ambazo waliuziwa na wananchi kwa shilingi milioni tano kwa ekari moja. Je huo ndio uwekezaji kweli? Kwanza hao wawekezaji waliouziwa ardhi hadi ekari 400 waliuzuwa kwa kazi gani?
Kuna mdau mmoja hapa jf aliwahi kusema kuna kijiji morogoro ambacho mwekezaji amekinunua chote! Mwekezaji kununua kijiji kizima kwa kazi uwekezaji gani?
Binafsi nina mashaka na nia za hawa tunaowaita wawekezaji, na matunda ya kuwauzia ardhi tutakuja kuyaona baadae/muda si mrefu.