Zanzibar: Uwekezaji kwenye ardhi wageuka mwimba mchungu kwa Wakazi, watumika kupora ardhi

Naahchina

New Member
Dec 6, 2016
1
0
Kwa miaka kadhaa sasa Uwekezaji umekuwa ukitumika kama njia ya uporaji ardhi kwa Wakazi wa Zanzibar, na hili linathibitika katika Kijiji cha Michamvi – Kae, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja kilichopo umbali wa Kilomita 41 kutoka Mjini, Unguja.

Kwa miaka 13 sasa katika Kijiji hiki ambacho shughuli kubwa za Wakazi wake ni Uvuvi na Kilimo, kumekuwepo na mzozo usiokoma wa umiliki wa ardhi yenye urefu wa mita 200 na upana wa mita 160, unaowahusisha Wakazi wa eneo hili na Mwekezaji kutoka Kampuni ya Dreams Sands ya Dar-es-Salaam.

Kutokana na mzozo huo, Mwekezaji amekwama kujenga Hoteli ya Kitalii huku hoja ikiwa ni malalamiko ya Wananchi kwamba Mwekezaji kajiongezea eneo, hadi kufikia kwenye ufukwe ambapo awali hakuwa akifika huko.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji, Vuai Iddi Mlenge, anathibitisha kwamba Wazazi wao waliuza eneo hilo kwa Mwekezaji, pasipo kuligusa eneo la upwa, ambalo anadai kwamba bado ni mali ya Kijiji.
1.jpg


“Wapo watu ambao walimuuzia, ila hawakuuza upwa wa bahari. Eneo lake lina alama, japo hakuna nyaraka za kuthibitisha hilo kwa upande wa Kijiji. Serikali inapendelea zaidi Wawekezaji na si Wazawa kwenye upatikanaji wa haki,” anaeleza Mlenge

Aidha, Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kusini kabla ya kuhamishwa, Rajab Yussuf Mkasaba, anautaja mgogoro kuwa ni jambo ambalo liko kisheria. Anasema “Mwekezaji yupo kisheria, ana hati zote na haki zote kwenye eneo hilo. Hivyo, Wananchi wanapaswa kuzungumza ikiwa kuna suala halipo sawa na si kuvutana,”

Serikali inavyolizungumzia suala hili

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Sharif Ali Sharif, amesema hadi sasa, ZIPA haijatoa kibali cha Uwekezaji na kwamba mgogoro kati ya pande zinazovutana umekwisha na wameshakubaliana juu ya suala hilo.

Wakati ZIPA ikidai kutokuwapo kwa mzozo katika eneo hilo, Wananchi wa Kijiji cha Michamvi – Kae wanasema bado wanaendelea kudai haki yao kutoka kwa Mwekezeji, ambaye amepata kunukuliwa akisema, hakuna wa kumzuia katika malengo yake ya kiuwekezaji zaidi ya Mahakama.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dream Sands, Lilian Kileo amesema ana nyaraka zote za kumiliki eneo hilo. Amesema “Mahakama ndiyo inayoweza kuamua kwenye suala hili. Lakini nitaendelea na utaratibu wa ujenzi. Nina ushahidi wa mauziano,”

Ameongeza, “Wakati wa kununua, hapakuwepo na mchanga, lakini kwa sababu karatasi zangu zinaonesha mbele napakana na bahari, basi ni eneo langu kihalali”.

2.jpg


Hali iliyo Zanzibar kuhusu migogoro ya ardhi

Katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 Mahakama ya Ardhi ilikuwa imepokea mashauri mapya 165, yaliyofunguliwa Unguja na Pemba. Kwa kipindi hicho hicho, mashauri 160 yalikuwa yametolewa uamuzi

Tangu mwaka 2015, Zanzibar haijaweka wazi suala la migogoro ya ardhi iliyopo katika ya sekta ya uwekezaji, huku takwimu zikionesha kwamba, nusu ya mashauri yanayotajwa migogoro ya ardhi, ni migogoro inayohusika na uwekezaji.
 
Back
Top Bottom