Hili la UDOM, Wizara ya elimu ina matatizo ya uongozi

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,257
2,882
Ukiangalia mgongano wa maelezo yaliyotolewa na Waziri wa elimu, baadauye akaja Rais Magufuli, baadaye afisa wa chuo na wengine wote wamekuwa na maono tofauti.

Tatizo langu ni kwa nini Waziri awe na uelewa tofauti na Rais. Niliamini sana kwamba kabla rais hajalizungumzia hili la UDOM, basi angepata uelewa toka kwa waziri wake. Pamoja na tofauti hizo nahisi kuna tatizo ktk uongozi wa wizara ya elimu. Inaonekana Rais aluipata maelezo tofauti toka kwa watendaji ndani ya wizara na bila kuficha katibu mkuu anaweza kuwa ni chanzo cha taarifa tofauti na ile aliyonayo waziri.

Wizara hii ina naibu katibu wakuu wawili, mmoja anashughulika na elimu ya juu na huyu ndiye namtilia mashaka sana. Siyo mara ya kwanza naibu huyu amevuruga mambo na kulalamikiwa hapa JF baada ya kufanya hivyo hivyo alipopelekewa matatizo ya SUA. Badala ya kuzungumza na waalimu ili kujua matatizo ya chuo, aliishia kufanya ’pati’ na uongozi wa chuo. Kwa UDOM naamini kabisa maelezo mabovu kwenda kwa rais ilikuwa ni njia ya kuuokoa uongozi wa chuo. Badala ya ubovu wa uongozi sasa suala limekuwa ni ufaulu duni wa Wanafunzi, jambo ambalo halipo katika wale 7000.

Hawa viongozi wa chuo pamoja na naibu katibu mkuu wa elimu ya juu wanastahili kuwekwa kado, nje ya wizara hii. Imani yangu ni kwamba naibu katibu mkuu hajaiva au hana uwezo kwa nafasi kama hiyo. Anaonyesha katabia kama mwalimu wa zamu anavyotawala wanafunzi.
 
Back
Top Bottom