Hili la pombe za viroba limekosa hoja zenye mashiko

Hili la pombe za viroba limekosa hoja zenye mashiko

Wakuuu salaam sana.

Leo ni siku ya pili tangu kutekelezwa agizo la serikali la kupiga marufuku uzalishaji pamoja na uuzwaji wa pombe zilizokuwa zikifungashwa katika mifuko ya plastic maarufu kama kiroba.

Agizo hili limekua ni la kukomoana na linapingana moja kwa moja na sera ya kutengeneza nchi yenye uchumi wa viwanda.

Wafanya biashara hawakutendewa haki na wateja wao pia.

1. Serikali ilitoa jumla ya siku 10 kwa wafanyabiashara na wazarishaji kusitisha biashara hiyo. Katika hili ni dhahiri itaonekana kulikua na ungwe ndani yake; ni vipi mzalishaji mkubwa anaweza kumaliza malighafi zote na kupata soko la stock yote ndani ya siku kumi??? Hivi hii serikali inadhani kuendesha kiwanda ni sawa na biashara ya genge?? Viwanda hununua malighafi za kutosha tena hata za mwaka mzima na kuziweka stock. Kumpa mzarishaji siku kumi asitishe uzarishaji ni uzandiki usiokubalika.
Ikiwa wauzaji wa rejareja tu wameshindwa kumaliza stock nadhani unaweza ku imagine namna gani hali mbaya kwa wenye viwanda/ wazalishaji.
Je hii ndo njia ya kuelekea uchumi wa viwanda?? Wale ndugu zetu waliokopa mtaji na kufanya biashara hii nini hatima yao???

2. Mamlaka husika zilipiga marufuku pombe za viroba kwa "kisingizio" eti zinaharibu mazingira. Sitaki kubisha hata kidogo katika hili ila ningependa tu kuwakumbusha si viroba pekee ndo hifungashwa katika mifuko ya plastic. Pia tuna...

×Ice cream za azam zinafungasha katika vifungashio vya plastic

×Maji safi ya chupa nazo ni plastic
×Mifuko ya plastic imesheheni tele madukani

Hebu tupite pamoja mashimoni na hata dampo...hebu tufanye upembuzi yakinifu pamoja....hebu tuangalie pasi na kupepesa macho..... Je ni kweli hiyo mifuko ya plastic iliyojaa huko ni ya viroba pekee?

Kama tumeamua kupambana kwa mazingira basi tufanye kweli ila kama mmeamua kuzuia viroba basi tuweke sababu wazi. Tusisingizie sababu za kimazingira.

NB Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya.

Mkandumbwe [emoji767]2017
Naomba niongezee kwa kuuliza kuwa serikali inaeza kutoa tathmini ya uharibifu wa mazingira tangu viroba wiwepo?
Viroba ambavyo vimekiwepo miaka yote hii unawezaje kuvizuia ndani ya siku 10?
Unawezaje kusema unajenga viwanda wakati huo huo unaua vilivyopo kwa nguvu kubwa?
Serikali inajua kodi inayokusanywa ktk viroba vya Konyagi na K Vant?
Mteja wa jumla aliyenunua mzigo mkubwa mwezi uliopita na akalipa kodi, anarudishaje pesa yake ili aendelee na biashara nyingine?

Kwa nini wafanyabiashara wananyanyasika ndani ya taifa lao?
Serikali inaleta ubabe na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda ili iwe rafiki wa nani?

Ila ni sawa tu, wacha tufundishwe adabu, tarehe 25 October 2015, kuna watu walifanya maamuzi ambayo wanayajutia leo. Ndiyo endelea kujuta, na baadae rudia tena. Utajuta wewe mpaka vijukuu vyako.
 
Wameambiwa wafungashe pombe zao kwenye chupa. Sasa ukiondoa sababu hizo za kimazingira, hayo madhara mengine mengi uliyosema sote tunayafahamu yatawezaje kuondoka kwa kubadili tu vifungashio?
unaweza kuweka chupa ya bia kwenye mfuko wa suruali au bapa la konyagi ,au kikopo dizaini ya maji uhai?
ukaingia nacho ofisini? ukaenda nacho shule? ukaenda nacho mihangaikoni? ukaweka mfukoni ukawa unaendesha boda boda?!!!

tunapunguza matumizi ya kizembe ya pombe!!! hata mahala pasipostahili kwa wakati usio stahili!!!
 
unaweza kuweka chupa ya bia kwenye mfuko wa suruali au bapa la konyagi ,au kikopo dizaini ya maji uhai?
ukaingia nacho ofisini? ukaenda nacho shule? ukaenda nacho mihangaikoni? ukaweka mfukoni ukawa unaendesha boda boda?!!!

tunapunguza matumizi ya kizembe ya pombe!!! hata mahala pasipostahili kwa wakati usio stahili!!!
Huo utetezi hauna nguvu, umekosa ukomavu. Kama solutions zenyewe tunazoweza kufikiria ndio hizo, basi tumekwama mapema. Bora tufungie kabisa pombe na sigara nchi hii zisitengenezwe wala kuuzwa.
 
Huo utetezi hauna nguvu, umekosa ukomavu. Kama solutions zenyewe tunazoweza kufikiria ndio hizo, basi tumekwama mapema. Bora tufungie kabisa pombe na sigara nchi hii zisitengenezwe wala kuuzwa.
wakishavinywa wakikimbiza mitaani na mapanga mnatupa lawama polisi
 
Back
Top Bottom