mkandumbwe
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 424
- 371
Wakuuu salaam sana.
Leo ni siku ya pili tangu kutekelezwa agizo la serikali la kupiga marufuku uzalishaji pamoja na uuzwaji wa pombe zilizokuwa zikifungashwa katika mifuko ya plastic maarufu kama kiroba.
Agizo hili limekua ni la kukomoana na linapingana moja kwa moja na sera ya kutengeneza nchi yenye uchumi wa viwanda.
Wafanya biashara hawakutendewa haki na wateja wao pia.
1. Serikali ilitoa jumla ya siku 10 kwa wafanyabiashara na wazarishaji kusitisha biashara hiyo. Katika hili ni dhahiri itaonekana kulikua na ungwe ndani yake; ni vipi mzalishaji mkubwa anaweza kumaliza malighafi zote na kupata soko la stock yote ndani ya siku kumi??? Hivi hii serikali inadhani kuendesha kiwanda ni sawa na biashara ya genge?? Viwanda hununua malighafi za kutosha tena hata za mwaka mzima na kuziweka stock. Kumpa mzarishaji siku kumi asitishe uzarishaji ni uzandiki usiokubalika.
Ikiwa wauzaji wa rejareja tu wameshindwa kumaliza stock nadhani unaweza ku imagine namna gani hali mbaya kwa wenye viwanda/ wazalishaji.
Je hii ndo njia ya kuelekea uchumi wa viwanda?? Wale ndugu zetu waliokopa mtaji na kufanya biashara hii nini hatima yao???
2. Mamlaka husika zilipiga marufuku pombe za viroba kwa "kisingizio" eti zinaharibu mazingira. Sitaki kubisha hata kidogo katika hili ila ningependa tu kuwakumbusha si viroba pekee ndo hifungashwa katika mifuko ya plastic. Pia tuna...
×Ice cream za azam zinafungasha katika vifungashio vya plastic
×Maji safi ya chupa nazo ni plastic
×Mifuko ya plastic imesheheni tele madukani
Hebu tupite pamoja mashimoni na hata dampo...hebu tufanye upembuzi yakinifu pamoja....hebu tuangalie pasi na kupepesa macho..... Je ni kweli hiyo mifuko ya plastic iliyojaa huko ni ya viroba pekee?
Kama tumeamua kupambana kwa mazingira basi tufanye kweli ila kama mmeamua kuzuia viroba basi tuweke sababu wazi. Tusisingizie sababu za kimazingira.
NB Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya.
Mkandumbwe 2017