HILI LA "MADE IN TANZANIA" LIMEKAAJE?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
1,163
1,125
Katika mkakati mzuri wa sera ya viwanda ya awamu ya tano lipo jambo ambalo naliona muhimu lakini halipewi umuhimu unaostahili.

Nchi inaweza kuzalisha na kuuza bidhaa zake sehemu nyingi duniani ila hazitambuliki kwa kukosa utambulisho.

Wafanyabiashara wengi wa nchi jirani wananunua bidhaa zilizozalishwa hapa nchini ila kinachonisikitisha ni bidhaa zetu kukosa utambulisho wa "made in Tanzania na bar code. Maandishi ya TBS yangekuwa na maana kama utambulisho ungetangulia.
Kama sheria ipo basi isimamiwe ipasavyo. Bidhaa isitoke kiwandani bila bar code na Made ni Tanzania kwa kuchapishwa kwenye kifungashio, kuwekwa mhuri au label ishonewe.

Ni wakati wa kutambuliwa kwa bidhaa zetu kwenye soko la dunia.

Na hao wanaotoa takwimu za market share wanazipataje wakati bidhaa hazina utambulisho?
 
Tatizo watanzania hamna jema.
TBS wakisimamia hilo jambo mnaanza kulalamika na kusema nchi Ina ukiritimba.
Kuna wengine walitoa uzi hapa siku chache zilizopita kwamba TBS wanataka kupiga chapa zao kwenye biashara ya mifuko mbadala watu wakaanza kulalamika na kusema wafanyabiashara wa kihindi wamehonga ili kuwakandamiza wafanyabiashara wadogo.
Kwa hyo wafanye lipi jema?
 
Back
Top Bottom