Hili la mabaunsa Dar kutumika kubomoa nyumba, si la kuvumilika

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,553
Hii inashangaza sana, Serikali ilichukulie kundi hili sasa ni hatari maana hawa watu wanaishi vipi ikiwa siku mojamoja tu ndio huenda kufanya uonevu kwa raia pengine wenye haki kabisa ya ardhi au eneo fulani?

Tukuombe Mheshimiwa Makonda baada ya ombaomba uwageukie hawa mabaunsa wamejaa mjini na nguvu zao kumbe serikali ingewatumia hata kwenye mashamba ya miwa huko Kilombero na Kagera hasa kipindi hiki cha uhaba wa sukari.

Nimesikitika kuona leo wamevunja nyumba za wanakijiji huko Pugu na familia zile zimebaki nje ati wanatetea ardhi ya mwekezaji. Jamani tafuteni shughuli zingine za kufanya!
 
Wamesahau wale wenzao waliochezea mikuki madale.. busara muhimu sana
 
hata mimi imenisikitisha sana.kwa mtu anayejua gharama na shida za kujenga hata chumba kimoja hawezi kabisa kuvunja nyumba ya mtu mwingine hovyo hovyo. utakuta hapo mtu kajenga kwa kuuza vitumbua miaka zaidi ya mitano huku anakula mlo mmoja kwa siku tena ugali kwa nyanya chungu halafu anakuja mtu na pesa zake na mabaunsa wake anavunja hiyo nyumba. naiomba serikali ichukue hatua kali ikiwezekana huyo mwekezaji na mabaunsa wote wakamatwe wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke na iwe fundisho kwa watu wengine wenye pesa wanaonea wasio na uwezo.
 
Ni jambo bays sana kuvunja nyumba za watu lakini na sisi wananchi kabla hatujajenga kwenye maeneo tunayouziwa tujiridhishe na uhalali wa eneo hilo. Hii nayo itaweza kupunguza haya mambo yanayojirudia sana.
 
Dhurma kubwa,na pengine hao wanakijiji wana haki zote kumiliki eneo husika,ila unajua tena rushwa imetaramaki,wenye pesa wanapindisha sheria wapendanyo...inasikitisha.
 
Hili sakata ukiliangalia haraka haraka limekaa kama uenda wazimu, lakini kwasisi tuliowahi kuingizwa mkenge na watu wa serikali za mitaa kwa masuala ya viwanja tunaamini kuna jambo linaendelea kimya kimya
 
Hili sakata ukiliangalia haraka haraka limekaa kama uenda wazimu, lakini kwasisi tuliowahi kuingizwa mkenge na watu wa serikali za mitaa kwa masuala ya viwanja tunaamini kuna jambo linaendelea kimya kimya
Mkuu uko sawa sana, kuna kitu hakijawekwa wazi vizuri. Mwenyewe niliwahi kupigwa na hao hao serikali ya mtaa huko Goba kuja kutahamaki tayari niko kwenye mgogoro wa ardhi iliyokuwa ndani ya wanafamilia. Ilibidi niwe mpole na kuongeza pesa kiasi ili nisipoteze kabisa.
 
Hao mabaunsa nao... C watanzania wengine tumezidi shobo.. Hv hatuon hata huruma wenzetu wanavopata tabu .. Cku iz kujenga hata choo ni mtihan mzito sana.. Sasa ww jitu unavunja kimjengo cha mwenzako eti unatetea ardhi ya mwekezaji... Co poa kabisaa.. sawa ngoja tuone action ya serikali.. !!!
 
Hawa watu wa Serikali za mitaa kama Hawajatumbuliwa kwa kuswekwa Jela basi Watabomo nyingi na zitaendelea kujwengwa nyingi.
Maana bado wanaendelea na kuuza mali zenye wawekezaji.
 
Back
Top Bottom