Hili la Loliondo Ole Sendeka alishinikizwa na Spika

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Tarehe 20 Juni, 2022 katika mjadala Bungeni, Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Olonyokie Ole Sendeka alijenga hoja nzuri sana ya kisheria kuhusu mgogoro uliopo katika eneo la Loliondo na Sale ambayo ilikuwa ni hoja ya msingi sana na hoja nyepesi sana kueleweka na mtu yeyote hata ambaye hajui sheria, ila kisheria na kimantiki ni hoja inayoeleweka ila hoja ya Ole Sendeka ilivurugwa na hivyo kufanya kwamba haina maana .

Eneo la Loliondo ni eneo lenye Kilometa za mraba 4000, Serikali imepanga kuchukua eneo la kilometa za mraba 1500 wakiita ni eneo la Pori tengefu (Game Controlled Area) tangu 1951 wakitaka kulipa hadhi kuwa hifadhi (Game reserve).

Mgogoro upo hapo katika kuchukua hilo eneo la kilometa za mraba 1500 kutoka katika eneo hilo la kilometa za mraba 4000 na wananchi waachiwe kilometa za mraba 2500.

Maeneo ambayo yapo katika hilo eneo la kilometa za mraba 1500 ni kata 6 ndani ya tarafa ya Loliondo (Arash, Oloipiri, Oloirien, Soitsambu, Ololosokwan , Loosoito ) zenye vijiji 24 na kata mbili katika tarafa ya Sale (Malambo na Piyaya ) .

Hoja ya kwanza maeneo haya yote ni miongoni mwa maeneo ya vijiji yaliyosajiliwa na kupewa HATI ya umiliki ,na umiliki wake upo chini ya mamlaka ya Serikali ya vijiji kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya 1923(kifungu cha 9) , hivyo maeneo hayo yalihama kutoka kumilikiwa kimila (Customary land) hadi kuwa maeneo yaliyosajiliwa na yenye Hati ya usajili na sheria ya 1923 kipindi cha ukoloni ilitambua usajili wa maeneo hayo ya vijiji.

Hata baada ya Uhuru ,Sheria ya Serikali ya mtaa Na.7 ya 1982 ,Sheria ya ardhi ya 1999 na sheria ya vijiji Na.5 ya 1999 kifungu cha 7(12), sheria zote hizi zimeendelea kutambua HATI za umiliki katika vijiji hivyo kwamba vinamilikiwa chini ya mamlaka ya Serikali ya mtaa. Hii ni hoja ya upande wa usajili ,umiliki na hati .

Katika upande wa sheria ya uhifadhi ya wanyamapori ,Sheria iliyoanzisha Pori la akiba la Loliondo ilikuwa sheria ya 1951 iliyoitwa Fauna Game Ordinance ,iliyoanzisha Pori la AKIBA katika ardhi ya Vijiji.

Mwaka 1974 ikatungwa sheria mpya ya uhifadhi ya wanyamapori iliyofuta sheria ya Fauna Game Ordinance ya 1951 . Sheria hii mpya ili tangaza maeneo ya Loliondo kuwa maeneo ya Pori tengefu (Game Controlled Area) ndani ya maeneo ya Vijiji . Sheria hii haikuondoa haki ya umiliki wa ardhi kwa wananchi chini ya mamlaka ya vijiji.

Mwaka 2009 ,ikatungwa sheria mpya ya Uhifadhi ya wanyamapori Na.5 ya 2009 iliyoanza kufanya kazi tar 7,Januari ,2010 .Sheria hii ya 2009 kifungu cha 122 ilifuta sheria ya wanyamapori ya 1974 .

Sheria hii mpya ya 2009 kwa kutambua maeneo mengi yaliyonywa kuwa Pori tengefu yalikuwa ni maeneo /ardhi halali ya wananchi chini ya Serikali ya vijiji ,Sheria hii ikaweka kifungu cha 16 kifungu kidogo cha (4) na (5) ili kutatua changamoto hii.

kifungu kikisema, " For the purpose of sub (section) ,the minister shall ensure that no land falling under village land is included under Game Controlled areas " .

Hii ina maana ya kwamba tangu sheria hiyo kuanza kazi baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali tarehe 7, Januari,2010 maeneo yote ambayo ni maeneo yanayomilikiwa na wananchi chini ya mamlaka ya Serikali ya kijiji (Village land) hayapaswi kuwa sehemu ya Pori tengefu ,yaani kwa lugha nyepesi sheria hii ilikuja kuondoa mapori tengefu yote kutoka katika maeneo ambayo ni ardhi za vijiji .

Maeneo yote ya hizo kilometa za mraba 4000 au hata hizo 1500 ni maeneo halali ya wana wananchi chini ya mamlaka ya Serikali ya vijiji yaani ni ardhi ya Vijiji ,kwa mantiki hiyo serikali au mtu yeyote yule anakosea kuita eneo hilo linalogombaniwa kwamba ni eneo la Pori tengefu ,sababu sheria imekataa ardhi ya vijiji kuwa sehemu ya Pori tengefu .

Hoja hizi ndizo ambazo Mbunge wa Simanjiro Mh.Ole Sendeka alikuwa anajiaribu kutengeneza na kuongea ,Spika Tulia alichofanya ni kumvuruga tuu Mh.Ole Sendeka kwa kumwambia amtajie kifungu kinachofuta hayo mapori tengefu hili lilikuwa shinikizo kwa Ole Sendeka kupelekea Ole Sendeka kufuta maneno na kuondoa hoja yake aliyoiwasilisha na kuisimamia.

Mh.Spika alitaka kifungu ambacho kimetamka kwamba Mapori tengefu ya Loliondo "yamefutwa" , Sheria imetamka wazi kwamba maeneo ambayo ni ardhi inayomilikiwa na vijiji (Village land) hayapaswi kuwa sehemu ya Pori tengefu na eneo hilo la kilometa za mraba 1500 linalogombaniwa ili kuchukuliwa na serikali, kwa mujibu wa sheria hii ya 2009 sio Pori tengefu tena sababu ni miongoni mwa ardhi ya Vijiji hivyo huwezi kuipandisha hadhi kwenda kuwa hifadhi ya wanyamapori ( Game Reserve) ikiwa eneo hilo sio Pori tengefu kwa mujibu wa sheria ya ya wanyamapori ya 2009 kifungu cha 16 (4) (5) .

Ila mbali na yote haya , Vijiji vinne ndani ya Tarafa ya Loliondo (Ololosokwan ,Arash , Oloirien na Kirtalo) ambavyo vipo katika hiyo kilometa za mraba 1500 inayogombaniwa kuchukuliwa na serikali vilifungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki (Arusha ) Mwaka 2017 kesi Na. 15 ya 2017 ,kupinga maamuzi ya kuchukua eneo hilo kilometa za mraba 1500 , mwaka 2018 Septemba 25 yaliyotoka maamuzi (Rulling) yaliyotoka katika Shauri dogo No.10 la mwaka 2017 , Maamuzi ya shauri hili yalitoa amri 3 .

1.Kuzuia serikali au mtu yeyote kuwaondoa wamasai kutoka katika eneo lenye Mgogoro yaani katika eneo la kilometa za Mraba 1500 hadi kesi ya Msingi itakapoisha .

2.Wasiwaharibie nyumba wala kuchoma mifugo ya wamasai .

3. Kuzuia serikali,maafisa wa Serikali na Polisi wasiwasumbue wala kiwatisha wamasai walio katika hilo eneo la kilometa za mraba 1500 hadi kesi ya msingi itakapoisha.

Ambapo ni kama maamuzi ya Mahakama ya Afrika Mashariki hayajafuatwa.Ukisoma Mkataba wa Afrika Mashariki ibara ya 38 ,inaagiza nchi Mwanachama kuheshimu maamuzi na Mahakama ya Afrika Mashariki ikielekeza "Council of Ministers" .

Hukumu ya kesi ya msingi No.15 ya 2017 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki itatolewa hapo J.tano tar 22 /Juni/2022 ,katika Mahakama ya Afrika Mashariki .

Serikali itumie majadiliano ili kutatua suala hili la Loliondo na Sale .


Abdul Nondo.
 
Sisi wa pande hizo tumeumizwa sana na hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii.
Sijui tunaelekea wapi kama nchi.
Nimeumizwa pia na maneno yaliyokuwepo katika taarifa ya Merry Masanja alipokuwa akimpa Ole Sendeka. Wizara ile ni kama haijui ilichokiandika. Ni kama haijui inachokifanya.
Wizara ile ipo katika mateka.
 
Asante sana Abdu Nondo, umeeleza vizuri kabisa. Kiufupi Spika Tulia alichofanya ni kumchanganya Ole Sendeka kwa kutumia pulpit bullying tactics.

Lakini ukweli ni kwamba serikali kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2009 inatambua kuwa Eneo la vijiji vilivyomo ndani ya hizo sqk 1500 Loliondo huwezi kuvifanya pori tengefu au hata hifadhi.

Na hii inatibitishwa na Waziri Mkuu Pinda aliyemwandikia barua mkuu wa mkoa wa Arusha wa wakati huo akimwambia asiwahamishe wananchi wa Loliondo kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Nashangaa serikali ya Samia inataka kuvunja msimamo huo wa serikali hiyohiyo kabla ya kubadili sheria.
 
Serekali iliyoko madarakani kwa kunajisi uchaguzi wazi wazi hakuna uwezekano ikatii amri ya mahakama. Nijuavyo mimi serekali zinazoingia madarakani kwa kupora uchaguzi huogopa nguvu ya umma tu na sio mahakama. Kama tutaendelea kuwa waoga tusigemee kupata haki yoyote kupitia mahakama, bali nguvu ya umma tu ndio suluhisho.
 
Serekali iliyoko madarakani kwa kunajisi uchaguzi wazi wazi hakuna uwezekano ikatii amri ya mahakama. Nijuavyo mimi serekali zinazoingia madarakani kwa kupora uchaguzi huogopa nguvu ya umma tu na sio mahakama. Kama tutaendelea kuwa waoga tusigemee kupata haki yoyote kupitia mahakama, bali nguvu ya umma tu ndio suluhisho.
Serikali iliyopo madarakani ni halali na imewekwa na wananchi na vyama pinzani vilishiriki,sema umeamua kuufungia ubongo wako.
Na LISSU kura azozipata tunajua
 
Serikali iliyopo madarakani ni halali na imewekwa na wananchi na vyama pinzani vilishiriki,sema umeamua kuufungia ubongo wako.
Na LISSU kura azozipata tunajua

Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Ukitaka kujua kuwa ule haukuwa uchaguzi bali uhuni kama uhuni mwingine, ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kama matokeo yale yapo.

Na ukitaka kujua ule ulikuwa ni uhuni, watanzania tunafikia 60, ila tume inasema iliandikisha wapiga kura 29m+! Toka lini watu wazima wakawa idadi sawa na watoto kwenye nchi yoyote ile? Huu ni ukweli wa wazi, acha uhayawani wa wazi uliofanyika wakati wa uchaguzi wenyewe. Niendelee kuweka ule ukhanithi wazi au umeshiba?
 
Tarehe 20 Juni, 2022 katika mjadala Bungeni, Mbunge wa Simanjiro Mh. Christopher Olonyokie Ole Sendeka alijenga hoja nzuri sana ya kisheria kuhusu mgogoro uliopo katika eneo la Loliondo na Sale ambayo ilikuwa ni hoja ya msingi sana na
Wamasai lazima wahame Ngorongoro. Tufike mahali tutofautishe binadamu na wanyama. Ukweli ni kwamba Ole Sendeka ndiye KUWADI wa wafanyabiashara wa Kenya wanaofugia ng'ombe zao ndani ya Ngorongoro. Maelfu ya ng'ombe waliopo pale siyo ya Wamasai wa Tanzania bali Wamasai wa Tanzania ni vijakazi tu wanaolipwa ujira.

Hiyo Sheria inawanufaisha wakenya na siyo watanzania
 
Naunga mkono wamasai wahamishwe. Lkn spika jitahidi kuwa spika. Usiwe mtetezi wa serikali bungeni.
 
Hapana Abdul, Ole alishindwa kujitetea vyema. Alizidiwa akili tu! It's obvious kum twist Tulia inabidi uwe mbobezi na ilikuwa ni pambano la heavy weight against light weight. Ole alikuwa na hoja akabanwa kishule shule akashindwa kuteleza
 
Hapana Abdul, Ole alishindwa kujitetea vyema. Alizidiwa akili tu! It's obvious kum twist Tulia inabidi uwe mbobezi na ilikuwa ni pambano la heavy weight against light weight. Ole alikuwa na hoja akabanwa kishule shule akashindwa kuteleza
Tulia: Taja kifungu kilichofuta

Hii katika bali ile ya kushtukiza ambaye angeweza kujibu ni Tundu Lisu na mtemi Chenge basi!
 
Serikali iliyopo madarakani ni halali na imewekwa na wananchi na vyama pinzani vilishiriki,sema umeamua kuufungia ubongo wako.
Na LISSU kura azozipata tunajua
Kwani ni Lissu peke yake aliyekua mgombea kwenye huo uchaguzi?.Matokeo ya ule ujinga hata walioshiriki kuufanya waliwahi kuuongea.sasa wewe ni nani hadi ubishane na jambo la wazi kama lile.Au umeamua kufungia ubongo wako.
 
Back
Top Bottom