Hili la "kulinda kura" sawa ila watangulie hawa

Hili la "kulinda kura" sawa ila watangulie hawa

IMG-20151016-WA0009.jpg
haya sasa wakati wewe unalazimishwa ukalinde kura, mwenye mtoto anae sema hivyo mwanae analinda bia
 
Hata kukiwepo maandamano mfano Arusha huwezi kumwona mke wa Godbless lema wala wanae.
Dar hivyo hivyo huwezi kuona wake wa akina tundu lisu,mbowe wala edwin Mtei.Wake zao na watoto zao wanakuwa nyumbani mahali salama watoto wa watu wengine ndio wanaingia nao barabarani.

Hii kauli ya kusema kulinda kura wanataka watoto wa wengine ndio watoke kulinda kura.Watoto wao watakuwa pengine paris ufaransa,au marekani au sehemu safi ya hewa safi na burudani wanaachia watoto wa maskini wa tunduma,mbeya,arusha,DAR nk ndio waandamane watiwe ngeu na polisi HALAFU WAISHIE KULIA KAMA HUYO

attachment.php

Picha ya kitu kingine kabisa
It is better to keep your mouth closed and let people think you are a fool than to open it and remove all doubt.
By Mark Twain



 
Mimi nina shughuli zangu nitapiga kura na kurudi home sitokaa kulinda kura kwani hiyo ni kazi ya Mawakala...
 
Unakaa mita 200 unalinda kura, ndani wakala wako anakubaliana na matokeo, unayapinga na unaandamana, polisi wanatii amri ya mkuu wa majeshi, unavyunjwa mguu na kutolewa jicho, unaswekwa rumande na sio hospitali,watoto na mke wako wanalia sana, mgombea anaapishwa.umetolewa rumande upo nyumbani ni mwezi unapita,mtoto wako anarudishwa nyumbani kakosa mahitaji ya shule,unaendelea kuugulia maumivu,mkeo amekuchoka anakusimanga maana alikwambia ukipiga kura urudi, anataka kuondoka,aliyek
wambia linda kura yupo bungeni anawapa poleni wale wote walioumizwa wakati uchaguzi na kusaini posho anatuma pesa za ada kwa mwanae anayesoma ulaya..
 

Ndio style wanayotumia kuwahamasisha vijana kulinda kura, vijana hawatakua kwenye akili zao za kawaida!
 
Last edited by a moderator:
Tanzania ina watu milioni 50, walinda usalama sidhani kama wanafika milioni. Kuliko kujifanya wajuaji ni bora busara kutumika tu, kwa sababu hata nyie mnaoshabikia walinda usalama kuumiza raia hamtabaki salama & familia zenu. Huo ndio ushauri wangu kwenu wewe mtoa mada na wenzako wote!
 
Mnaifiza sio, sisi waTz wa kweli kulinda kura lazima. Hamtotugeuza wana Lumumba
 
Kila mmoja natamani kuona uchaguzi ukiwa wa huru na wa haki ili mwisho wasiku Tanzania ipate kiongozi bora.. Ila kila chama kina simammisha wakala zaidi ya mmoja hii ni kuhakikisha kua kunakua na ulinzi wa kutosha.. Sasa napata mashaka na hawa wachache wanaosema watalinda kura, unawezaje kulinda kura wakati uko umbali wa mita 200? huoni kinachoendelea ndani?

Ombi langu ni moja tu, watanzania wnzangu tuilinde amani yetu...wachche wasituvurugie mani yetu kwa amnufaa yao...
 
Hapo ukipata manundu ata pole upati wakalinde wao na watot wao
 
Kulinda kura ni kazi ya mgombea na familia yake
 

Attachments

  • 1445343642779.jpg
    1445343642779.jpg
    33.2 KB · Views: 199
kura tutazlnda,ili tuwaondoe madiwani wabovu wa ccm,bila kusahau na wabunge wa "ndiyooooo",pamoja na kumwondoa na kutokumweka raisi anayehubiri kuwa ata wafunga mafisadi ila akashindwa kutimiza vitendo!
hao watoto wa mbowe and co,wawepo wasiwepo sio sabb ya kususia kuzilinda kura!kwani mke wangu akilazwa sakafuni hosptalini kwa kuwa niliogopa kulinda kura kwa kuwa watoto wa viongozi hawakuwepo bado itakula kwangu!hao watoto wa wakubwa baba zao washinde au lah bado bata watakula tu!ila mie maskini pona yangu ni sanduku la kura!
 
Jibu ni jepesi mno,hivi lowassa na upinzani kwa ujumla wakishindwa uchaguzi na ccm ikaendelea kutawala na wananchi tukaendelea kupigika,je,hao uliowataja wataathirika pia?Sisi malofa tutalinda kura kuiangamiza ccm,amani ya mioyo yetu itatulia pale ccm itakapokaa bench!Hatuwezi kudanganyika tena,kwanini jeshi la polisi halitaki kufanya ulinzi shirikishi kwenye suala hili?Kama polisi watakubaliana na wananchi washirikiane kulinda kura ni jambo jema,atakayeshindwa ataridhika kuwa ameshindwa kihalali!Miaka iliyopita watu tulilinda kura na hakuna uvunjifu wa amani uliotokea,iweje iwe nongwa Leo?
 
Lakin kama uchaguz utakuwa wa Haki kwa nn ccm wanaogopa sana jambo hili?

Hakuna mtu aliekataa mambo ya kulinda Kura.Ila kura zinalindwa na mawakala tena wanaoteuliwa na Chama chenyewe.Sasa kama humwamini mwanachama wako then unamwamini nani???!Halafu Chadema ni watu wa vurugu sana hawaaminiki hata kidogo.Kuna vyama vya siasa 18 vinavyoshiriki uchaguzi mwaka huu-ukiruhusu wafuasi wao wote walundikane vituoni ni chanzo cha FUJO NA VURUGU.Mbona upinzani umekuwa ukishinda majimbo ya KARATU,MOSHI NA KIGOMA kwa haki tu
 
Na huyu yumo kwenye kundi la wasomi wa chuo kikuu puu!!ndio maana Tanzania hatumo hata kwenye 30 vyuo bora Africa, EL anakuambia kipaumbele ni ELIMU,ELIMU ELIMU umejichoraje??
 
Kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa hili nimeiona post yenye hekima kubwa mnoooo, big up mtoa mada.
 
IBRAHIM MGAYA

Kulijua hilo kunahitaki akili ambazo hawa ndugu zetu wamezikosa kwa muda mrefu...
 
Last edited by a moderator:
Itabidi tufanye kampeni ya kuhamasisha viongozi wa vyama pinzani kwenda kulinda kura pamoja na wanachama wao kama wanavyowataka wafanye
 
kulijua hilo kunahitaki akili ambazo hawa ndugu zetu wamezikosa kwa muda mrefu...

ama kweli akili ni nywele na ninavyoona wenzetu tangu wamezaliwa hawajawahi ota nywele mpaka leo
 
Back
Top Bottom