Hili la "kulinda kura" sawa ila watangulie hawa

Hili la "kulinda kura" sawa ila watangulie hawa

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,609
Kwa muda sasa kumekuwa na mjadala wa kile kinachoitwa "KULINDA KURA" na kwa kuwa muda mwingi niliutumia vijiji vya Mbeya nikifanya kazi tukufu ya kuwahubiria neno la kweli wananchi wa nchi hii iliyobarikiwa ya Tanzania kuwa mabadiliko ya kweli yapo ndani ya CCM na kwamba wamkatae shetani na wafuasi wake kwa kukataa wala rushwa na mafisadi wa nchi hii, walioliangamiza Taifa hili kwa miaka mingi kwa uroho na ubinafsi wao.

Kwa kuwa sasa "kazi hiyo takatifu" imeshatimia, na wanambeya wamenielewa, sina tena shaka na maamuzi yao ifikapo October 25, hivyo nimepata fursa ya kurudi tena kujumuika na wanajamvi wengine kujadili hoja na vioja mbalimbali vinavyoletwa hapa Jamvini kila uchao.

Kwa mtazamo wangu, sioni tatizo kabisa kwa watu kulinda kura zao, hata ikiwa watu hao wanataka kukaa sentimeta moja kutoka ilipo kura hiyo, nasema hivi nikiamini kuwa kura ni mali kama zilivyo mali nyingine hivyo ulinzi wake ni jambo la msingi sana.

Na nawaunga mkono Viongozi wa Upinzani wale "wanaoshadidia kuwa kura zao lazima zilindwe" na wanasisitiza kuwa hawamuamini yeyote hata wasimamizi wa kimataifa..nasema ni sawa tu ikiwa tutawaona wao wakiwa mstari wa mbele kulinda kura hizo kama walivyo mstari wa mbele kuhimiza Ulinzi huo.

Ila matukio na taarifa (ambazo baadhi nimeshazithibitisha na nyingine bado ni tetesi) zimenipa mashaka juu ya dhamira halisi ya hiki kinachoitwa KULINDA KURA.

1. Taarifa za kuhamishwa kwa mabilioni ya fedha kutoka kwa Viongozi wakuu wa UKAWA, wahisani na wadau zimenistua kidogo, nikijiuliza kwanini mabilioni hayo yahamishwe sasa..??? kwanini yanakimbizwa nchini..? Napata mashaka kuwa watu hao wanajiandaa kuanzisha makazi mapya na maisha mapya kule ambako zimehamishiwa fedha hizo.

2. Taarifa za safari za familia za Vigogo hao wa UKAWA nazo zinatia mashaka, taarifa za safari ya Mke wa Maalim Seif Sharrif Bi Awena Sinani Masoud pamoja na mtoto wake wa kike kuondoka nchini tarehe 16 Oct 2015 zinaukakasi, kwanini waondoke wakati huu, vipi kuhusu haki yao ya kupiga kura..? Vipi kuhusu himizo la kulinda kura..? Ama wao sio wahusika ama walengwa wa mpango huo..?

3. Safari ya Franklin Frederick Sumaye kwenda Hosuton, Texas nchini marekani hivi karibuni, inanifanya kuhoji uelewa wa umuhimu wa "kura" kwa Viongozi wa UKAWA hata waruhusu watu walio na uhakika kuwa watawachagua waondoke katika kipindi hiki, ina maana hawazihitaji kura zao, ama hawaitaji ulinzi wao..?

Mimi nasema na kuendelea kusisitiza kuwa suala la Kulinda kura ni "HAKI" ya kimsingi kabisa ya yeyote yule, hivyo CCM wanayo haki hiyo na vyama vingine pia..lakini wale wanaohimiza jambo hili tunataka kuwaona wakilinda kura hizo pamoja nasi, tuzione familia zao zikilinda kura zao..sio sisi kajamba nani..!!

Nataka wafuatao wawe vinara wa kulinda kura katika vituo walivyojiandikisha, ili na sisi wengine tukalinde zetu katika Vituo vyetu..namaanisha hawa wafuatao kwenye picha hizi;

21.jpg

Familia ya Mgombea Urais wa UKAWA Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa, ikiongozwa na Fred wawepo vituoni kulinda kura zao na za baba yao.

attachment.php

Bi Awena Sinani Masoud na mwanaye wa Kike, wawepo Vituoni mwao walinde kura zao na za baba wa familia yao.

BHewsAQCAAAm2h1.jpg

Kijana wa Miaka 22, Clinton Freeman Mbowe (kushoto) itapendeza kama ataongoza kundi la walinda kura kituoni kwake.




Najua jambo hili litaibua fikra kama zangu katika baadhi ya vichwa vya wanajamvi humu ndani lakini pia najua nimealika mvua ya matusi na maneno ya shombo kutoka kwa wale jamaa zangu wa "kazi maalumu" wa kule ngome, mtaa wa maguruwe - Mbezi na wale wa pale kituoni Ufipa. Lakini vyovyote iwavyo sitaacha kufikiri na kushirikisha wenzangu katika fikra zangu.

Wanaposema tukalinde kura, nafahamu kuwa wanamaanisha hawa hapa chini kuwa ndio walinzi wa kura zao..

CRr0zOwWoAAP-Qa.jpg

Kwa ulinzi wa ndugu zangu hawa, sidhani kama "salama" itapatikana. Ila vyovyote iwavyo nawatakia kila la heri kwa "mpango huu"
 
Tutatumia style ya Mijizi ya CCM, usijali na haya mambo hayakuhusu. Kama walivyoiba kwenye Escrow, Kagoda, Meremeta n.k
 
Lema naye tumuone akilinda hizo kura maana pesa zinahamishwa tu na hatuelewi matumizi yake!
 
Hata kukiwepo maandamano mfano Arusha huwezi kumwona mke wa Godbless lema wala wanae.
Dar hivyo hivyo huwezi kuona wake wa akina tundu lisu,mbowe wala edwin Mtei.Wake zao na watoto zao wanakuwa nyumbani mahali salama watoto wa watu wengine ndio wanaingia nao barabarani.

Hii kauli ya kusema kulinda kura wanataka watoto wa wengine ndio watoke kulinda kura.Watoto wao watakuwa pengine paris ufaransa,au marekani au sehemu safi ya hewa safi na burudani wanaachia watoto wa maskini wa tunduma,mbeya,arusha,DAR nk ndio waandamane watiwe ngeu na polisi HALAFU WAISHIE KULIA KAMA HUYO

attachment.php
 
Hakuna sheria inayomruhusu mwananchi au mpiga kura KULINDA KURA!Sheria inasema watu wakae mita 200 sawa na urefu wa viwanja viwili vya mpira wasubiri matokeo!!na sio kulinda kura!

Kazi ya kulinda kura ni ya POLICE na Mawakala wa vyama
 
Haendi mtu kulinda kura kwa hali hii, hwa jamaa hawana practical train wakikushukia wanamaliza hapo hapo, tulinde amani watanzania kwa kufuata sheriatu
polis.jpg
 
Back
Top Bottom