Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliliambia Bunge kuwa kuanzia Septemba mosi mwaka huu, itakuwa ni marufuku kwa mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi kusimama vichakani ili abiria wao wajisaidie haja kubwa na ndogo maarufu kama kuchimba dawa. Mwakyembe alitoa agizo hilo mwezi uliopita wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara yake na kueleza madhara yanayotokana na vitendo hivyo vya kuchimba dawa vichakani.
- Kwanza, Dk. Mwakyembe alisema ni kitendo cha udhalilishaji kisaikolojia, hasa kwa wanawake, kuvua nguo hadharani mbele za watu wakiwamo watoto wao ili kujisaidia.
- Pili, akafafanua kwamba mbali na kadhia hiyo, pia ni hatari kwa usalama wa abiria hao kwani huko wanakopelekwa kujisaidia si sehumu salama, wanaweza kukumbana na wanyama wakali wakiwamo nyoka hivyo kudhurika.
- Tatu na kubwa, Waziri Mwakyembe alisema vitendo hivyo vinaharibu mazingira, hivyo kuhatarisha usalama wa afya za wakazi wanaoishi jirani na maeneo husika, na kwamba serikali haiwezi kuvumilia kuendelea kukaa kimya.........
Tunadhani ipo haja ya wizara yake kushirikiana na wenye mabasi yaendayo mikoani, kuhakikisha vinajengwa vyoo vya umma katika maeneo mbalimbali kutegemeana na urefu wa njia ambavyo vitawekewa usimamizi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kufanyiwa usafi. Vyoo hivi vinaweza kujengwa jirani na vituo vya kuuzia mafuta vilivyopo jirani na barabara au karibu na makazi ya watu halafu vikakabidhiwa kwenye usimamizi wa uongozi wa eneo hilo na wenye magari pamoja na serikali wakawa wanachangia gharama za matunzo na usafi. Baada ya hatua hizo kufanyika ni rahisi sana agizo la Waziri Mwakyembe kutekelezeka kwani kutakuwa na mbadala wa vichaka, abiria nao hawawezi kukubali tena kupelekwa huko wakati wanajua vipo vyoo mahala fulani..............
MWAKIEMBE AMEKURUPUKA BILA TATHMINI YA MAANDALIZI YA KUTOSHA
Kwa maoni yangu kauli ya Waziri Mwakiembe ni ya kukurupuka bila kujipanga, la sivyo angeleta upembuzi yakinifu namna gani serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo kwa kushirikiana na umoja wa wenye mabasi nchini, au serikali yenyewe ingejipanga kivyake tu kama ilivyo kwa nchi nyingi.
Barabara kuu maeneo ya mwendo mrefu ambayo hayana restaurants kando yake, serikali inatakiwa kujenga vituo vya kupumzikia, si kwa wasafiri wa mabasi tu, ila kwa magari yote kuanzia usafiri binafsi, magari ya abiria na mizigo.
Maeneo hayo ambayo hujulikana kama REST AREA huwa na huduma muhimu ya vyoo, vitafunio na vinywaji kwa kununua, ingawa nchi nyingine vyoo kwa vile vimejengwa na pesa ya walipa kodi huwa havilipiwi ila vitafunio na vinywaji. Huwepo parking ya magari madogo na makubwa, ulinzi wa watu na mali zao na wahudumu.
Baada ya serikali kujiridhisha kwamba imeandaa maeneo hayo, hakungekuwa na pingamizi kuchukuliwa hatua za kisheria anayekiuka utaratibu wa kuchafua mazingira kwa kuwa sehemu za kupumzikia na restroom vimeandaliwa. Lakini kwa sasa vita hivyo si rahisi kushinda kutokana na maandalizi yasiyofanyika kwa kiwango na hasa kutegemea vituo vilivyopo vya watu binafsi bila kufikiria maeneo yenye umbali mrefu ambayo hayana huduma hizo.