Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,711
- 1,738
Nawasifu TRA na TCRA kwa msimamo wao wa kusimamia EFD na ving'amuzi. Jambo lolote lianzapo huwa na kasoro zake hasa linapohusu pesa kwa maana ya kudhibiti mianya ya wachache kujineemesha. TFF inanishangaza kwa kusimamisha (bila muda maalum) matumizi ya 'electronic tickects' tena kinachonifadhaisha zaidi ni kuwa rais wake, Jamal Malinzi, ndio mhusika haswa wa kusitisha matumizi hayo. Ilipaswa TFF ing'ang'anie jambo hili wakati wakirekebisha kasoro zilizojitokeza. Ndipo ninapoona labda pana haja ya bunge kutoa maamuzi ya kurejesha tiketi hizo kwani ni dhahiri mtindo huu wa sasa ni kunufaisha watu binafsi na sio kuendeleza soka nchini.