Kama kweli mada zote zinazoletwa hapa jukwaani na wadau mbalimbali ni za kweli..basi,ni bora hata mchakato wa katiba mpya usitishwe tu..sisemi kwa nin mchakato wa katba usitishwe ila kwa mwenye akili ameishaelewa ninachokimaanisha hapa.
Lengo ni kwamba kuna watu wamekumbwa na mikasa tofauti tofauti, ikiwezekana hata kubakwa lakini hawatodiriki kuja jukwaani kusema yaliyowajiri itabidi waendelee kuumia moyoni na hawajui namna ya kuondokana na ile hali sababu imeshawaathiri kisaikolojia. Sasa mtu anaweza akaja na mada nimebakwa utotoni mwangu, au nimebakwa siku chache zilizopita haina maana kuwa yeye amebakwa kweli, hapana, ni moja ya kuwasaidia wahanga(waliobakwa kweli) kutokana na kusikia mkasa labda kutoka popote katika jamii inayotuzunguka.
Kwa hapa mleta mada anakuwa amewasaidia wahanga indirect, unajua kivipi?
Ni pale wachangiaji watakapoleta maoni yao na wahanga wakayapitia inawasaidia kwa namna moja ama nyingine