QUALIFIED BIOLOGY TEACHER
Member
- Oct 27, 2024
- 33
- 277
Pole haya ni mapito tu wala hayadunu miaka yote.Toka nakuwa na ufahamu nimeona wazazi wangu wakipambana sana, lakini bahati haijawa upande wetu, mama kavunja sana kokoto, baba nae kapambana sana lakini wapi.
Wazazi wangu wamenisomesha kwa shida sana, hadi chuo kikuu ambapo serikali ilinipa mkopo, wazazi walitegemea sana niwe mkombozi wa familia Baada ya masomo. LAKINI imekuwa tofauti Sana.
Toka mwezi wa Saba nimemaliza, nimejaribu kupambana kutafuta kazi ya fani yangu ya ualimu lakini pote napokwenda nakosa, application zaidi ya kumi na sita lakini wapi.
Nimejichanganya mitaani, wakuu Kila kazi napiga lakini malipo ni madogo sana , kazi takutumia nguvu hazina malipo mazuri kabisa. Pesa inaishia nyumbani, na mahitaji ya wadogo wangu, wazazi wamechoka sana na umri wao umeenda Sana
Kwa wiki napata kazi mara mbili tena hapo Kwa kutafuta na hungaika sana, malipo ya saidia fundi huku kwetu ni elfu Saba siku nzima.
Napesa yenyewe haikai, natoa sapoti nyumbani ( maisha yetu ni kama msumari na nyundo ).
Sina mtu, Wala ndugu anaweza nishika mkono au kunipa mtaji , ikifika jioni najikunja nakuwaza sana. Hii kitu inaniuma sana Sana.
Nawaza hivi kwa maisha haya kweli tatoboa, Kweli takuwa na mafanikio. Bahati Mbaya ajira zenyewe ngumu I feel too bad 😓😓😓
Ushauri mzuri sanaUtatoboa tu mkuu,endelea kujichanganya. Kwanza ulifanya kosa kubwa sana kusoma ualimu. Hiyo hata ukiajiriwa kwa hiyo kazi bado utakua masikini kama ulivyo sasa. Kwa ustawi wako,zingatia yafuatayo;
1.Unamudu vizuri kuendesha gari,pikipiki,bajaji na Guta
2. Uwe mchapakazi kwelikweli. Ishi kama hukuwahi kwenda shule ila ktk michongo yako ipige kisomi kiwango cha Phd
3. Kuwa na nidhamu isiyotia mashaka ktk kazi zako. Weka nidhamu ya kiseminari
4. Kuwa muaminifu 100%. Usijaribu wala kuwaza kuiba,kudhukumu na kuhujumu cha mtu
5. Jijengee uwezo wa kujichanganya nq matajiri au watu waliofanikiwa kukuzidi. Kama una tabia tajwa hapo juu hutokosa majukumu na kipato cha kusurvive kisha mdogo mdogo utaaminika kwenye michongo
6. Ukianza kupata michongo tumia akili na uwezo wako wote kuanzisha kitu chako! Kaa mbali kabisa na kampani za ulevi na umalaya
7. Muombe sana Mungu na kutoa sadaka kwa mujibu wa imani yako ktk hatua zako zote kuanzia sasa
Nakutakia kila la heri mkuu. Ni wewe wa kuikomboa familia yako kiuchumi na sio mtu mwingine. Ukishindwa tutakulaumu wewe. Hilo sitaki kukuficha mkuu! Kila kitu kinawezekana ukiamua na kukubali kulipa gharama hitajika
Umaskini huzaa umaskini. Wazazi wako walijua hawana uwezo na wakajiona wao ni mabingwa wa kutotoa watoto kama kuku anavyototoa vifaranga. Matokeo yake ni kuwa wamekubebesha mzigo wa kulea wadogo zako. Ushauri wangu ni kwamba kwenye maisha, kukata tamaa ni adui namba wani kuliko umaskini wenyewe. Soma vitabu ujifunza watu wenye ulemavu na matatizo mengine walivyoweza kupambana na kuwa matajiri.Toka nakuwa na ufahamu nimeona wazazi wangu wakipambana sana, lakini bahati haijawa upande wetu, mama kavunja sana kokoto, baba nae kapambana sana lakini wapi.
Wazazi wangu wamenisomesha kwa shida sana, hadi chuo kikuu ambapo serikali ilinipa mkopo, wazazi walitegemea sana niwe mkombozi wa familia Baada ya masomo. LAKINI imekuwa tofauti Sana.
Toka mwezi wa Saba nimemaliza, nimejaribu kupambana kutafuta kazi ya fani yangu ya ualimu lakini pote napokwenda nakosa, application zaidi ya kumi na sita lakini wapi.
Nimejichanganya mitaani, wakuu Kila kazi napiga lakini malipo ni madogo sana , kazi takutumia nguvu hazina malipo mazuri kabisa. Pesa inaishia nyumbani, na mahitaji ya wadogo wangu, wazazi wamechoka sana na umri wao umeenda Sana
Kwa wiki napata kazi mara mbili tena hapo Kwa kutafuta na hungaika sana, malipo ya saidia fundi huku kwetu ni elfu Saba siku nzima.
Napesa yenyewe haikai, natoa sapoti nyumbani ( maisha yetu ni kama msumari na nyundo ).
Sina mtu, Wala ndugu anaweza nishika mkono au kunipa mtaji , ikifika jioni najikunja nakuwaza sana. Hii kitu inaniuma sana Sana.
Nawaza hivi kwa maisha haya kweli tatoboa, Kweli takuwa na mafanikio. Bahati Mbaya ajira zenyewe ngumu I feel too bad 😓😓😓
MkuuUmeelezea lakini ungesema umesoma ualimu wa science au wa arts astashahada, stashada, shahada kwasababu kuna watu wengi humu pengine ungepata msaada.