Hili jambo la kukejeli waomba ushauri/ msaada liangaliwe upya

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
7,447
13,189
Wanasema 'Internet' ndio sehemu pekee unayoweza kumwambia mtu jambo ambalo usingeweza kumwambia ana kwa ana. Ni kama tunavyomuita Magufuli Pogba ama Jiwe. Ila sidhani kama miongoni mwetu kuna ambaye ana uthubutu kumuita hivyo mheshimiwa ana kwa ana.

Mimi sio mkubwa kihivyo ila nashukuru nimeanza kutumia mitandao ya kijamii kabla hata sijafika miaka 15. Enzi hizo nachat thegrid ile ya vodacom na mitando mingine. Point yangu sio kuonesha ukongwe wa mitandao hapana point ni kuwa nina 'experience' japo sio sana ya members wa mitandao ya kipindi hicho na kipindi tulichopo. Zama hizi masihara yamekuwa mengi. Mimi ni mmojawapo wa wapenda masihara kama kuna mtu anafuatilia posts zangu. Lakini ninachoshukuru natambua wapi nifanye masihara wapi nisifanye.

Maisha ni fumbo kubwa. Umezaliwa una wazazi wawili mshukuru Mungu. Viungo vyako vya mwili vyote vinafanya kazi mshukuru Mungu. Akili yako iko vizuri mshukuru Mungu. Unajimudu mahitaji yako yote ya msingi mshukuru Mungu.

Kuna mahali fulani muda huu tunavyoongea hapa kuna mtu anatamani apate hata robo ya robo ya ulichonacho lakini ndio hivyo.

Hatukatai matapeli wapo lakini na wa kweli pia wapo. Hata makanisani au misikitini tuna uhakika gani sadaka zetu zinaenda kutumika sehemu sahihi? Kama wasimamizi wa sadaka wataamua kuila basi na dhambi itakuwa juu yao huku wewe fungu lako la haki likihidhiwa sehemu salama kwa kuwa umetimiza wajibu wako.

Bado sijajaliwa kipato cha kuweza kuwainua na wengine na ndio maana nikiona uzi wa mtu anaomba msaada ni kheri nikakaa pembeni au nijitahidi kwa namna yoyote ile niandike kitu positive. Maumivu ya kukejeliwa nayajua, maumivu ya kukosa pesa ulipohitaji kuliko wakati mwingine nayajua. Kuna aliandika kitu sio kizuri kuhusu muomba msaada fulani nikamuuliza utajisikiaje siku unakutana na huyo mtu unagundua hakuongopa?

Kama huna nia ya kumsaidia mtu ni kheri ukae pembeni kuliko kukatisha tamaa wanaotaka kujitolea. Yaani unamuomba mtu adisclose taarifa zake binafsi, ushahidi kuwa yuko kwenye shida anafanya vyote unavyotaka halafu unalala mbele. Basi angalau rudi kwenye uzi waambie watu ni kweli huyu mtu anahitaji msaada nao utakuwa ni msaada tosha.

Anyway kuna mengi ya kusema ila tuombe hekima wakati wote.

Wanasema ukitaka kuwa na busara fanya hivi:

"Fikiria jambo lolote la kipumbavu halafu ukishalipata kaa kimya usiliseme."
 
Tatizo kundi kubwa la watu siku hizi wanatumia mitandao ya kijamii kulinganisha maisha ya watu tofauti tofauti na yake. Ndio maana Utakuta Instagram kila mtu anataka onekana kama superstar kumbe sio uhalisia
Hili hupelekea watu wengi kuishi maisha wakiamini kila mtu yupo hivyo. Ndio maana ukipata pesa ukaomba ushauri wa biashara lazima mtu atachukulia kama unajidai au utapeli, ukiwa na shida anaamini unaigiza au utapeli au shida yako inatatulika
Shida nyingine linapokuja suala kama hili kila mmoja hujiona halimuhusu anaesemwa ni mtu mwingine. Hivyo tubadilike hili jamba linatuhusu sote
If you want to change the world begin by changing yourself first.
 
Back
Top Bottom