Hili fumbo lina maana gani..?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,214
56,853
Ardhi iliotesha mti,mti wa mauwa na matunda naam mti wa mauwa na matunda wenye asali na achali na ndege waasiliyo waliootesha vichali waishio wao na watoto wao.
ukijani umelemetao wapendeza kwa ndege hao,kama sumaku ivutayo waasiliyo hutua matawi watakayo tena pasi mashaka waasiliyo hula nakusaza!.
Upepo kutoka mbali ukaleta ndege wakali wakaanzisha vichali wenye ushupavu na uhodari wakuruka mpaka mbali,wenye midomo hatari yenye miba na misumari,waasili wakaa mbali kwa kuogopa makali ya ndege walojivika majani ya mti!
Mti umedumazwa,mauwa yametandazwa,matunda yameondoshwa waasili walia kimvuli kimepotea!

fumbo hili lina maana gani..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom