Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Huu ni ushauri ambao nadhan ingekuwa vyema kama serikali yangu haitojali kuufanyia kazi. kila mkoa kungeanzisha free zone area ambako huko watu wangekuwa wanaruhusiwa kwenda na kuongea yote waliyo nayo moyoni halafu wakimaliza wanarudi na kuendelea na mambo yao.
hii ingesaidia sana kuwatua watu mizigo waliyo nayo moyoni kutokana na msongo mkubwa wa mawazo walio nao na hali mbaya kiuchumi waliyo kuwa nayo toka miaka mingi iliyopita na mwendelezo wake.
kwa wale ambao watajisikia wakienda hapo wakamseme vibaya Rais au mawaziri wake,wabunge n.k waruhusiwe iwe ni eneo ambalo wanaweza wakasema lolote lile watakalo. wawekewe viti,sehemu ya kununua vinywaji pia na kasehemu ambako wanaweza wekewa sanamu moja kubwa la kupiga mawe ikiwa watajisikia uchungu zaidi. sanamu hilo lisiwe na sura ya mtu yeyote ila liwakilishe kila aina ya mtu ambaye mhusika atatamani ampige mawe. hii itapunguza hata matukio ya kumrushia mawe Rais kama ilivyotokea kwa kikwete.
watu wana chuki sana mioyoni mwao wnaposikia tembo wanauawa,twiga wanasafirishwa,vifaru wanaibwa,sukari inapanda,madawa ya kulevya yanashamiri,watoto wa wakubwa wanajitajirisha kwa kupitia kodi za wananchi maskini,mbuga za wanyama zinauzwa,migogoro ya ardhi,madini yao yanachimbwa kwa bei ya kutupwa,pesa zao zinagawanywa kwenye viroba,magunia ya lumbesa,mifuko ya sandarusi n.k, manunuzi hewa, wafanyakazi hewa, wafanyabiashara flan kukwepeshwa kodi n.k
mnadhan haya machungu wakatolee wapi? wapewe sehemua ambayo wataweza nao kupasua majipu yao ya moyoni. waachiwe nafasi nao huko wakatupe mawe kuwatupia mashetani waliowafanya wao waishi maisha kama wapo jehanam. hii itasaidia kupunguza msongo wa mawazo, hasira na chuki.
wakienda hapo wawe huru hata kumwita rais wa taasisi fulani shetani, wamwite majina yote wanayotaka, wakiwa hapo wawe na ruhusa hata kumuita mkurugenzi,mbunge,waziri,boss shetani au bwege. wakitoka hapo wawe wamemaliza hasira zao. bila hivyo miaka kadhaa ijayo magereza yatakuwa hayatoshi. yatajaa watu waliomtukana rais wa taasisi flan,mkurugenzi n.k
nami pia kwa kuandika haya natoa ruhusa kwa wenye msongo wa mawazo kuanza kunitukana pasipo kusita. wanitukane tu itawasaidia kupunguza msongo huo.