Hili bango linatukebehi wana Dar

Hili bango linatukebehi wana Dar

Kwa hali hii ya maji, hili bango la kampeni ni kama kebehi kwetu sisi wananchi.

Wahuni ndani ya ccm wasichojua ni ule ukweli kuwa tuko siku za mwisho; hata kama watafanikiwa kuwanyamazisha watanzania, bado hawataweza zuia ratiba ya Mungu kutimia. Yesu alionya kuwa siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu. Aidha, bibla inaonya kuwa ubinafsi utatamalaki na hasa kwa wale wenye mamlaka. Kibaya zaidi, inasema watatoka kutoka ubaya mpaka ubaya zaidi, wakidanganya na wao wakidanganywa.
HAPA NINACHOSISITIZA ni kwamba, hali ngumu kama ukosefu wa mvua, uchumi wa dunia kudorora, vita na majanga mengine ya kidunia hatuwezi kuyaepuka katika siku hizi za mwisho. Matokeo yake Raia wataanza kujilinganisha jinsi wanavyoathirika na namna viongozi wao wanavyoendelea kufaidi maisha; hapo ndipo hasira za wengi zitaelekezwa kwa watawala.
Mkumbuke ule mwaka 2000 ambao dunia iliusubiriaga, wakati tunaenda mwishoni mwa 1999, kiukweli dunia haikuwa imelinganisha calendar yake na calendar ya Mungu kuhusu MASIHI. Mwaka halisi ambapo inatimia miaka 2000 tokea Masihi kutokea duniani ni mwaka 2029!! Mwenye akili na ang'amue hilo.
Si ajabu haya yaliyotukuta hapa Tanzania yakawa ndiyo mwanzo wa UTUNGU (uchungu wa uzazi) mark my word; hali zetu Tanzania zitatoka toka mbaya mpaka mbaya zaidi.
Hamna nafuu, kama kutoa ushauri, ni bora mtu kuwaachia wengine waendelee nalo. Mama litamshinda si kwa sababu ya watu anaowanyamazisha, bali hawezi kupingana na unabii wa siku za mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom