Hiki ndicho walichokivuna Chadema

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,520
86,081
Kwa kifupi zifuatazo ni faida za UKUTA ambazo zimepatikana kwa maslahi mapana ya Upinzani na Taifa kwa ujumla. Waweza kuongeza za kwako, hii ni analysis kwahio mods msiichanganye na mada nyingine. Naomba

Moja, Serikali na Polisi wake wamesaidia sana kukitangaza chama kwa gharama zao wenyewe! Kwenye hili Chadema hawakulipia hata tangazo labda kununua vifurushi vya TV tu ili kusikiliza taarifa.

Pili, kwa mara ya kwanza Polisi wamepata nafasi ya kufanya mazoezi ya viungo kwa zaidi ya mwezi mzima na hivyo kuwasaidia kiafya na kikazi, wale wenye vitambi nina uhakika vimepungua kwa kiasi flani, pia imesaidia Polisi kununuliwa baadhi ya vitendea kazi ikiwepo uniforms, ni jambo jema.

Tatu, JWTZ watafanya usafi nchi nzima kesho, Oooghh what a blessing? Nadhani hawataahirisha kufanya usafi. Nchi imekua chafu kwahio mitaro itazibuliwa kesho na hivyo kupunguza magonjwa ya milipuko.

Nne, imesaidia media kukaidi agizo la Nape kuwa wasiripoti mambo ya UKUTA Ila the opposite is true, hakukua na habari za Blaza Yohana wala CCM.

Narudi tena....
 
Back
Top Bottom