Hiki ndicho nilitaka kusoma, siyo hizi porojo zenu kuhusu kusimamishwa kwa Mch. Dkt. Kimaro

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,774
21,270
Na Askofu Bandekile Mwamakula.

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Wakush...
FB_IMG_1660506252228.jpg


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Tokea lini Askofu wa Morovian akawa na data ama resolutions za vikao vya kiitifaki vya maaskofu wa KKKT?

Huyu ameongea maoni yake kama anavyoongea mambo yake mengi yansiyo katika wito wake wa Injili.

Mimi nasema kuwa Wakristo ni wachache mnooo kuliko hao wanaiita Wakristo kwa mapokeo na misingi ya dini.

Njia ile ya Uzima ni NYEMBAMBA, waionao ni wachache na waipitao ni wachache. Maana yake kati ya watu mia wanaofanikiwa kuiona ni kumi na wanaofanikiwa kuipita ni watano.

Safari ya kwenda Mbinguni siyo nyepesi kama tunavyofarijiana na maneno ya kuhamasishana huku matendo yetu yakituhukumu kuwa si watakatifu.

Ndugu zangu.
Tusimuogope Mungu bali tutafute kwa bidii kumkaribia kwa sababu hakuna anayeweza kumsogelea hadi awe amewezeshwa na hatuwezi kuwezeshwa ikiwa hatumuombi uwezo.
 
Ndugu Msanii kama umesoma alichoandika huyo Mwamakula unaweza kurekebisha andiko lako upya, although iwe sijui uhamsho, mara KKKT au AIC wote wapo kwenye kapu moja la umoja wa madhehebu nchini, so huwezi kukashifu ukristo alafu utegemee msabato binafsi akugombeze!.
 
KKKT mjifunze kuokoka, kwani akisema vijana wa kiislama ni waaminifu kuliko wakiristo anamaana gani katika kuhubiri? Shida ipo kwenye uelewa wa injili. Mchungaji alikua na maana ya ninyi kubadilika.
Hata wachawi mbona ni waaminifu kuliko wakiristo kwasababu wanatoa sadaka kubwa na wanafanya maombi muda wote tena usku wa manane sis tukiwa tumelala. Nikikufundisha hivyo simaanishi mchawi amekuzidi. Namaanisha ubadilike Ile ufanye maombi ili uwashinde.
 
KKKT mjifunze kuokoka, kwani akisema vijana wa kiislama ni waaminifu kuliko wakiristo anamaana gani katika kuhubiri? Shida ipo kwenye uelewa wa injili. Mchungaji alikua na maana ya ninyi kubadilika.
Hata wachawi mbona ni waaminifu kuliko wakiristo kwasababu wanatoa sadaka kubwa na wanafanya maombi muda wote tena usku wa manane sis tukiwa tumelala. Nikikufundisha hivyo simaanishi mchawi amekuzidi. Namaanisha ubadilike Ile ufanye maombi ili uwashinde.
Na hii thread inatakiwa iishie hapa maana point imepatikana👏🏼
 
We tend to glorify our differences more than those aspects that unifies us.

Religion is a mental slavery.

Dini ni utumwa wa kifikra kwa waafrika... poor Africa!
Kimaro ameongea ukweli mchungu kwa watu lazima atapigwa vita tu kama ilivyokuwa Yesu Kristo.
 
Migogoro kama hii huwezi ikuta Roman Catholic ni huko huko pembezoni kwa watu wenye sharubu, ndevu na watutumua misuli
 
Back
Top Bottom