Mwanasiasa mkongwe nchini, Stephen Wasira amesema kilichomfanya aamue kumvamia mwandishi wa gazeti la Mwananchi juzi ni kitendo cha kupigwa picha nyingi alizoona zimekithiri.
Wasira, ambaye aliingia kwenye siasa mwaka 1970, alipigwa picha hizo wakati akitoka kwenye jengo la Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara mjini Mwanza ambako shauri la wakazi wa Bunda waliokuwa wakitaka kukata rufaa ya kupinga ushindi wa Mbunge Ester Bulaya wa Chadema katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015, lilitupwa.