Hiki ndicho alichosema Dr. Lwaitama

DR Lwaitama alijibu mapigo yaliyotolewa na Rais, na viongozi wa chama cha mapinduzi, alisema mambo yafuatayo;

  1. CDM wana haki ya kutafuta na kuongeza wanachama kwa kuzunguka mikoani, haki hiyo ni ya kikatiba na vilevile ipo chini ya Sheria Ya Vyama vya Siasa.
  2. Na CCM kama inahitaji ifanye hivyo, isikalie kulalama tu
  3. Mambo yanayoongelewa na CDM ni halali kwa sababu kazi ya chama cha siasa ni kuangalia mambo ambayo yanayoumiza wananchi
  4. Hakuna machafuko yoyote kwa sababu, CDM walipoenda Mwanza walifanya mikutano baada ya pale wananchi wapo wanendelea na shughuli zao kama kawaida, vivyo hivo Shinyanga, Kagera na Musoma
  5. Maandamano yote yalipata baraka zajeshi lapolisi lakini pia walipewa ulinzi wa polisi sehemu zote
  6. Hakuna anayewalazimisha wananchi kuhudhuria mikutano ya CDM bali wananchi wanavutwa na kukunwa na sera za CDM, Hivyo CCM isiwasemee wananchi
  7. Wanaotaka kuvuruga hii nchi ni CCM kwasababu ya kuendeka swala la Amani ambayo mda wote imekuwepo
  8. Maneno ya Chiligati, RAIS, waandishi wa habari ni kutaka kukisaidia chama cha mapinduzi ili kuweka taswira kwa wananchi kuwa CDM ni mbaya inaleta vurugu, hivyo kuwafanya jeshi la polisi wasiruhusu maandamno ya CHADEMA kanda za juu kusini
  9. Hakuna aliye na lengo la kupindua serikali, bali Serikali legelege huondolewa kwa maandamano madogo kwa sababu serikali ya namna hii huogopa kila kitu ni hutaka kudhibiti maandamano, likitokea hili serikali husababisha vurugu na hivyo kusasbabisha vita
  10. Aliwambia kuwa kama wanaona Mbowe na Slaa ndo wanasababisha vurugu ambayo haipo basi wawakamate na kuwatia ndani ili waone kama amani itakuwepo.
Haya ndiyo yaliyosemwa na Dr huyo, wewe una maoni gani?
naunga mkono hoja kwa asilimia 100%
 
Back
Top Bottom