Hii ya Shibuda Maswa imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ya Shibuda Maswa imekaaje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by makoye2009, Oct 27, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Baada ya mgombea Ubunge jimbo la Maswa Magharibi Mhe. Shibuda kuachiwa na polisi kuwa hahusiki na mauaji,Kamati ya maadili ya Uchaguzi ya Wilaya hiyo imemjia juu Shibuda kwa kutaka aenguliwe na NEC baada ya kuandika barua kwenda NEC.

  Kitu kinachoshangaza ni hii Kamati ya Maadili inaposhondwa kutumia busara. Kuwa Shibuda hahusiki na mauaji hayo na Polisi wamethibitisha hivo na ndiyo maana wakamwachia huru aendelee na Kampeni.

  Ni dhahiri kwamba Kamati hii iko kwa ajili ya maslahi ya CCM. Hilo liko wazi kabisa. Haiwezekani wafuasi au mashabiki wa vyama husika vya siasa wafanye vurugu na kuuana halafu useme mgombea wa chama mojawapo anahusika na aenguliwe. Hivi je,kama tukio hili lingekuwa kinyume chake Kamati hii ingelikuwa tayari kusema Wagombea wote wa CCM waenguliwe???

  Naamini NEC si wapuuzi kiasi hicho cha kukubaliana na maoni ya Kamati hii ya Maswa ambayo inataka kuibeba CCM kwa mbeleko kuipeleka Bungeni. Haikubaliki asilani.
  CCM wanaonyesha kuwa na hasira na uchungu na Shibuda kwa kuihama CCM bbada ya kumfanyia mizengwe kwenye kura za maoni ilhali bado anakubalika na wananchi.

  Hata kuwekwa ndani kwa Shibuda ililkuwa ni shinikizo la Vigogo wa CCM akiwemo Makamba,Kinana na JK. Hapa CCM wanaonekana na kuwa na siasa za chuki.

  Mimi nawakumbusha CCM tu kuwa wasifikiri tumesahau kile kilichotokea Zanzibar uchaguzi wa 2000 walipoua wananchi zaidi ya 25 kwa upuuzi wa maelekezo ya CCM. Mbona CCM hawakuenguliwa baada ya Polisi kuua idadi hiyo ya watu kwa maelekezo ya vigogo wa CCM? Chondechonde CCM na NEC msitake kurejesha mambo ya mwaka 2000 huko Unguja.
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  The Golden Rule : He who has the gold, makes the rules.
   
 3. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ondoa shaka. NEC hawawezi kuwa wapuuzi kiasi hicho. Watatupilia mbali ujinga huo. Hamasisheni tu wananchi wampe kura nyingi Shibuda.

  Pamoja na upuuzi alionao ki-LOVE hawezi kukubaliana na hayo ya kikamati cha madili hapo maswa
   
 4. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Halafu wamejuaji kama mgombe a wa CCM hakuhusika katika hizo vurugu? na hao vijana wake walikuwa wanatafuta nini maeneo ya kampeni za CHADEMA? Sometimes huu ni umbumbu wa kutafakari mambo kiundani.
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,642
  Likes Received: 21,854
  Trophy Points: 280
  Wamemuona Shibuda kuwa analeta fujo na kushauri aenguliwe wakimuhusisha na tukio ambalo hakuwepo, ila yule Mgombea aliyempa kipigo Kamanda wa jeshi letu la Polisi wilaya (OCD) ndiye anayefaa maana alikuwa ana mpa mazoezi kamanda huyo? kufanya kazi ndani ya unafiki ni aibu kwelikweli maana heshima inashuka.
   
Loading...