Kuna hil swala mie sioni kama limekaa vizuri na lina tija mbele ya watanzania ambao tunahitaji maendeleo na mustakabali wa nchi yetu. Tunafahamu kila chama cha siasa kina msemaje wake kwa mambo yote yanayohusu chama husika mfano CCM yupo NAPE NAUYE, CHADEMA yupo John Mnyika, sasa inapotokea kiongozi mwingine wa chama anaongelea mambo fulani hata yale ya binafsi halafu kutoka na kusema eti chama fulani wamesema kitu fulani mie naona sio sawa na ifike mahala tuweze kutofautisha kauli za chama na kauli za mtu binafsi. Mbona kauli za chama huwa zinakuwa na kichwa cha khabari kabisa?? Ni hayo tu kwani kila mtu ana uhuru wa kuongea na kutoa maoni yake ila tu asiingilie uhuru wa mtu mwingine kwani uhuru wa mtu unapoishia hapo hapo ndipo unapoanzia uhuru wa mtu mwingine.