MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Tangu vikao vya bunge la bajeti vianze CCM mmejiingiza kucheza ngoma msiyoijua na mtaicheza kweli kweli.
Mmeshindwa kuishauri mamlaka inayompa nguvu na kiburi Naibu Spika kuelewa kua kuwatimua wapinzani ndani ya bunge kwa kigezo cha vurungu si suluhisho bali ni kuibua mambo mapya, mmeshindwa kuishauri mamlaka inayoliagiza jeshi la polisi kuandama vyama vya vingine siasa kwa kigezo cha vurugu mkijua ndio wanashikishwa adabu, mmeshindwa kutumia wingi wenu ndani ya bunge kuzikubali hoja za upinzani zenye tija mnaleta ushabiki mkijua ndio ushindi wenu.
MTAMBUE YAFUATAYO ZIWE MBIVU AU MBICHI, LIWE GIZA AU NURU.
Mtambue kua kutaka kuudhibiti upinzani ambao nyuma yake kuna watanzania milioni 6 itawapasua vichwa maana hampambani na mtu mmoja ama wawili, mnataka kutujengea chuki ndani ya jamii ambayo ilizoea hali ya utulivu,busara na kuheshimiana.Kuzuia mikutano ya kisiasa kwa kuwaambia watu kua sasa ni muda wa kazi sio siasa nani kasema? Hilo halitawezekana na halitokaa liwezekane kamwe.
Mjue kua wenzenu ndani ya uponzani pamoja na tofauti zenu za kiitikadi nao ni wanadamu, nao wanaumia kama ninyi, nao wana familia kama ninyi, nao wanapenda kuheshimiwa kama ninyi, mnavyopenda vyeo nao pia hivyo hivyo kama ninyi. Hivyo msifikiri kua watakubali kurudi nyuma au watachoka kwa figisu figisu zinazofanywa na jeshi la polisi, zaidi ni kuwajengea usugu wa kuendelea kupambana na uonevu Kwa kutafuta njia mbadala.Hakuna mbunge wa upinzani atakayefurahia kupoteza nafasi yake ya kuwatetea wananchi kwa sababu tu ati CCM hawampendi, atapambana kwa namna yeyote ile kwa utaratibu wa kisheria na kikatiba kuhakikisha kua anatetea nafasi yake.
Sasa watanzania ndio wanapata uelewa kwamba ni nani mwanzilishi wa fujo katika taifa letu, Kwa sasa bunge linaendeshwa kiloloni, halina vionjo vya aina yake Kama bunge, halina taswira ya kibunge yaani lipo lipo utafikiri ni semina ya kitaasisi flani hivi.Hili watanzania wameshaliona wanatazama muda tu.
Hakika kitendo hiki kitendo cha CCM kutaka kubaki wao ndani ya siasa za nchi hii kutawapoteza hamtakaa msahau milele, hakuna wananchi watakaowaependeni, mtabaki peke yenu. Kukataa kukosolewa hamtayatambua mapungufu yenu, ndipo mtakavyojifukia vizuri.