Wakati vyama vingi vinaanza tulitumia kanuni ya mpinzani atatoka CCM, kanuni hii imefeli. Sasa hivi mpinzani wa kweli lazima azalishwe na upinzani

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tulipoaminishwa CCM itauwawa na wana CCM kutoka CCM kwenda upinzani ilikua sahihi kwa wakati huo kwa sababu watu walikua watiifu kwa chama na walipikwa kwenye chama nakufahamika nje ndani ya maisha yao.

Tukawa na waasisi akina Mrema, Slaa, Shibuda, Cheyo, Makani na wengine wengi waliojiengua CCM kuunda vyama vya upinzani.

Baadaye ikatumika kanuni yakupandikiza watu wa CCM kuunda vyama kuonyesha Dunia tuna vyama vingi sana na hivyo tuna Demokrasia. Mfumo huu umekuwa ukifanya kazi hadi sasa ambapo utaona vyama visivyo hata na mgombea mmoja mwenye nguvu yakushinda udiwani vinakutana na kutoka na maazimio yakumsimamisha mgombea urais mwenye nguvu kufanya kampeni. Kanuni inayotumika ni waliopandikizwa kusimama kama wapinzani wa vyama vikubwa kwa lengo lakuifanya ccm isiyumbe.

Kanuni hii inafanya kazi kwenye taasisi za vyama vya siasa ila haifanyi kazi kwenye miyoyo ya wananchi maana uwezi kuweka mapandikizi kwenye miyoyo ya wananchi bali utawarubuni watu wachache ambao wengi wao hawana ushawishi kwa jamii, hivyo kimfumo utaona una nguvu ila kisiasa huna nguvu maana mwanasiasa mtaji wake ni watu na si taasisi.

Kanuni ya Kwanza ya CCM to upinzani baada yakufa imezaliwa kanuni ya wapinzani bora kifikra na kimtizamo kuondoka upinzani kwenda CCM. Hii ndiyo kanuni inayotengeneza kifo cha CCM. Kwanini? Kwa sababu zifuatazo:

1. Wapinzani hawa hawaendi CCM kwa hiari Bali wanaenda kwa kusaka ajira, kushinikizwa, kuepuka kudhurika nk. Mtu wa namna hii uwezi kumwamini ukampa dhamana bila kumwekea mtu nyuma maana anaweza kusaliti wakati wowote.

2. Watu Hawa wanaokwendaCCM wana uwezo mkubwa wakufikiri na kupambanua mambo kuliko walippo CCM, hivyo wanakwenda kuchukua nafasi za ajira. Hii inawafanya wengi wa wapinzani wanapotaka kutimiza malengo binafsi wakaze buti upinzani ili wasajiliwe.

3. Upinzani nao umeaandaa mapandikizi, baadhi wanajijua kwamba wanafanya nn na baadhi wamekwenda ila wanajulikana wakati wowote wanaweza kurejea walipokulia.

4. Kupokelewa kwa wageni kumeua morali na nguvu ya vijana na viongoz wa CCM, awajui watadumu kwa muda gani hapo walipo. Kwa hasira na kuonyesha wanakerwa walidhihirisha kupitia walioitwa WAJUMBE. Waliwafyeka wote wakiotoka upinzani, hivyo wageni wanajua huko walipo hawapendwi. Wapo kwa kudra ya baba.

Sababu zilizoelezwa hapo juu zinatufundisha wanadamu kuwa na msimamo. Lissu anakula matunda ya uvumilivu, Mbowe anakula matunda ya uvumilivu, Bashe anakula matunda yauvumilivu, Mdee the same nk. Upinani wa kweli hautoki CCM bali unatoka upinzani , Membe usiaminishwe kua bado mpasuko utaletwa na wanaCCM Bali utaletwa na wapinza halisi na waliovaa ngozi ya CCM.
 
Sasa huyu msaliti wa Nchi Lissu naye ni mpinzani ?

Upinzani wake hautaacha legacy yeyote Tanzania, zaidi ya kutesa familia yake
 
Back
Top Bottom