Huo ni utapeli. Jambo la kwanza wanalifanya na kulitumia zaidi wana hack account za Facebook. Hivo wewe utadhani kweli ni jamaa yako ndo kakutumia.Lakini unakuta yeye mwenye account haoni kinachoendelea mtandaoni na kama huamini mcheki umwulize kama anajua kinachoendelea.
Pili ukishaingia kwenye hiyo link utakuta wametenga makundi ya hela kama unataoka milioni moja kiingilio ni kiasi fulani, nk.
Hebu mwulize huyo jamaa yako kama kweli yeye ndo kakutumia, malengo ya hizo hela zinazoitwa UNICEF FOUNDATION ni nini? Na wanapewa watu wa aina gani? vipi mfano watanzania wote milioni 60 wakaomba je hao wanaojiita UNICEF FOUNDATION wataweza kuwapatia?
Mwisho kwa taasisi kama UNICEF haiwezi kufanya vitu bila kuwa published kwenye official website yao.
Ahsante sana HYPERSONIC
ni jamaa yangu ninayemuheshimu sana alinitumia message kama ifuatavyo
''Kuna nambari ya Facebook messenger nataka nikutumie alafuu unitumie hapa sawa namba yangu iko na shida sawa''
mimi nikamuandikia ''ok tuma''
yeye kaandika ''uniandikie hapa sawa''
mimi ''sawa''
yeye ''umeona''
mimi ''sijaona kitu''
yeye ''sawa''
mimi ''sijaona kitu''
yeye ''sawa''
mimi ''tuma kama message ya kawaida''
yeye ''Alafuu umesikia kuhusu UNICEF promotion ama bado hauna habari''
mimi ''nasikia kijuu juu labda unipe details''
yeye ''wanapeana hela kiwango cha 3,464,000 si ujaribu mimi nimepewa''
Baada ya hapa akanitumia message ya alivyotumiwa Chaguo la Lipa na M-PESA kununua bidhaa ili kulipia message ni ndefu kama zile unapomtumia mtu hela au kutuma siwezi andika yote.
mimi sasa wewe ukipewa si utakuwa nawe ulichangia?
Baada ya hapo akanitumia link
yeye ''gusa hiyo mchongo inakupeleks na utex kwa Whatsapp''
Kiukweli sikusita kubonyeza hiyo link maana nilikuwa najua ninachofanya ikatokea sasa whatsapp inaniambia unatakiwa ujiunge na whatsapp link ambayo iko nje ya member wako sasa vile nilikuwa najua huu ni utapeli nikaacha ku accept nilibulshit
Ajabu jioni kwenye simu yangu nikatumiwa msimbo nikaambiwa huu ndio msimbo mpya wa facebook yako sikufanya chochote zaidi ya hapo ni kaachana nao sababu najua
Najitahidi nimtafute huyu jamaa yangu nimuulize
Nimeona nitoe haya kupitia hapa wana JF wenzangu tupeane tahadhari