Hii tabia ya kum-Tag mtu inakera sana

Hii tabia ya kum-Tag mtu inakera sana

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
Kwanini unaandika post au unaweka picha mtandaoni halafu unatag watu 100? wengine wanatag hadi zaidi. Mtu amepost picha anakula ugali na "kabichi" huko kwao Runzewe halafu anamtag kuanzia mwalimu wake wa shule ya msingi hadi mmiliki wa Facebook mwenyewe Mark Zuckerberg. What the essence?

Au unakuta mtu yuko Peramiho wala humfahamu halafu amepost picha anaandika "Im feeling sick with Malisa and 100 others." Una kichaa? Kwahiyo mimi na hao watu 100 wote tunaumwa pamoja na wewe?

Post yako inatakiwa "ijiuze" kwa content sio kwa idadi ya watu uliowatag. Kama post ina content nzuri hata usipomtag mtu itasambaa yenyewe kama moto wa kiberiti nyikani. Lakini kama umepost "mashudu" hata utag watu wote kuanzia Kibaha kwa Mathias hadi Tegeta kwa Ndevu bado haitasomwa.

Kutag msururu wa watu kwenye post ni ulimbukeni. Wakati mwingine unakuta mtu hahusiki na hicho ulichokiandika wala hakujui lakini umemtag. Unaongelea habari za huko kwenu Kibakwe lakini unatag watu walioko Tarakea. Ushamba.!!

Usitag watu kupata "likes" nyingi, usitag watu kupata "comments" nyingi. Unawakera hata kama hawakuambii. Mtag mtu kwa sababu anahusika na hicho ulichopost. Ukinuna jipige kifuani mara 3 kisha sema "mimi ni mjinga sana". Fanya hivyo kutwa mara 3 utapona.!!

Credit: G. Malisa
 
Mtu anapo Ku tag ujue amekuheshimu, au anajua wewe ndiyo mwenye uwezo wa kutatua tatizo au kutoa msaada mahali husika..
 
Mambo ya Facebook kuyaleta Jf ni ujinga. Kanungila Karim
IMG_20200605_110158.jpg
.
 
Back
Top Bottom